GET /api/v0.1/hansard/entries/1049220/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1049220,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1049220/?format=api",
"text_counter": 240,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Mimea hii inatufanya sisi tutambulike kama Wapwani. Tulipokuwa wadogo, mkorosho ulikuwa unafanya vizuri sana katika eneo la Pwani. Tulikuwa na kiwanda kilichokuwa kikisimamiwa na Serikali Kuu kilichojulikana kama Kenya Cashewnuts Limited. Kiwanda hicho kilikuwa kimetoa motisha kwa wakulima wengi wadogo wadogo katika eneo la Pwani waliokuwa wakipanda mkorosho kwa wingi. Leo hii, ni jambo la kusikitisha na kutamausha kuona mkorosho umesahaulika na umekufa. Hii ni kwa sababu kile kiwanda muhimu tulichokuwa tukitegemea hakifanyi kazi tena. Jambo la kushangaza ni kwamba baada ya kiwanda kile kuanguka kule Pwani, kilifufuka kule Thika. Leo hii korosho kutoka Pwani hununuliwa na middlemen ambao huenda kuziuza kwenye kiwanda ambacho kiko mjini Thika kinachojulikana kama Afrimac Nut Company. Hili ni jambo la kusikitisha. Kiwanda cha mkorosho kilikuwa Pwani, na watu wa huko walikulia. Leo hii The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}