GET /api/v0.1/hansard/entries/1049221/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1049221,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1049221/?format=api",
"text_counter": 241,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "mkulima anaingia gharama kubwa. Korosho zetu zimekuwa ghali mno kwa sababu ya usafiri mrefu. Kuhusu mumea mnazi, tumeambiwa kwamba uko na faida zaidi ya kumi na moja. Mbali na faida kubwa inayojulikana, ambayo ni pombe ya mnazi, kuna mafuta ya nazi yanayojulikana kuwa tiba. Tumeambiwa na watafiti kwamba mafuta ya nazi yanatibu saratani. Kuna mnazi unaotoa makuti. Ukienda kwenye hoteli zetu za kifahari, utaona vile mapaa yao yameekezwa na makuti ambayo yanaonekana kuwa nadhifu na ya kupendeza. Ukiukata mnazi, unatoa mbao nyingi sana ambazo hutumika kwa ujenzi. Kwa hivo, mnazi uko na faida nyingi sana lakini ni mumea mmoja ambao umesahaulika na Serikali yetu. Hatujakuwa na hata kiwanda kidogo cha kushughulikia mumea wa mnazi. Kama tulivyoskia hapa, kilimo ndio uti wa mgongo wa Jamhuri ya Kenya. Tunajua kwamba kilimo huchangia asilimia 30 ya Bajeti ya Serikali Kuu. Pia tunajua kwamba kilimo kimeajiri zaidi ya asilimia 70 ya Wakenya, ambao hutegemea sekta hiyo kwa maisha yao ya kila siku. Jambo la kushangaza ni kwamba wakati tunaposoma Bajeti, au wakati mipango ya Serikali inapofanywa, kilimo huorodheshwa kama nambari kumi. Barabara, usalama na sekta nyingine chungu nzima zimepewa kipaumbele ilhali uti wa mgongo wa uchumi wa nchi hii, ambao tunajua unategemewa na asilimia 70 ya Wakenya, imeorodheshwa nambari kumi. Tunaiomba Kamati ya Bunge hili inayohusika na masuala ya kilimo iangalie jambo hili. Sisi ndio tunaopitisha Bajeti ya Serikali. Ni lazima tuamue. Kama tunafahamu umuhimu wa kilimo ni lazima, kama Bunge la Taifa, tuekeze zaidi kwenye sekta ya kilimo ili sekta hii iimarike irudi kama ilivyokuwa zamani. Tumezungumza mambo ya mabwawa au zile tunaita katika Kizungu ukiniruhusu dams . Serikali imewekeza zaidi katika kuhakikisha tumejenga madimbwi yale ili mvua itakapokuwa imekuja, yale maji yasipotee bure. Sisi kama Wapwani tuna bahati kuu. Tuna mito miwili mikuu katika Jamhuri ya Kenya; Mto wa Tana ambao unaanzia milimani na unaishia Bahari ya Hindi. Tuko na Mto wa Athi River ambao unapitia maeneo ya Ukambani na unafika pale Sabaki na unateremka mpaka Bahari ya Hindi. Lakini wakati tumepata mvua ya kutosha, maji haya yote yanaishia katika Bahari ya Hindi. Lakini tukiweza kujenga vidimbwi hivi huko katikati, tunaweza tukachuma maji yale na yakatusaidia wakati wa ukame na tukahakikisha ukulima unakua katika maeneo mengi sana katika Jamhuri ya Kenya. Katika Pwani tumekuwa na mmea wa pamba. Tulikuwa na kiwanda kule Lamu kinajulikana kama Lamu Cotton Ginnery. Kiwanda kile pia kimekufa na kilikuwa kikipatiana mchango mkubwa sana kwa wakulima wadogo wadogo wa pamba kutoka maeneo ya Mpeketoni. Tumekuwa na kiwanda cha mkonge pale Vipingo Sisal. Kilikuwa kimeajiri zaidi ya watu elfu tano. Leo, kiwanda kile kimekufa na yale mashamba yote makubwa leo yamerudi mikononi mwa watu binafsi. Wanagawanya na kuuzia wananchi. Kwa hayo, naunga mkono Mswada huu. Asante sana."
}