GET /api/v0.1/hansard/entries/1049851/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1049851,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1049851/?format=api",
"text_counter": 57,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Omanga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13175,
"legal_name": "Millicent Omanga",
"slug": "millicent-omanga"
},
"content": "Bw. Spika, namalizia kwa kusema kwamba afya ni jambo la--- Shida ambazo tumekuwa tukiona katika Wizara ya Afya zinafaa kupewa kipao mbele. Madaktari wetu wanalalamika kwamba hawalipwi vizuri. Hatuna madaktari maalum wa ugonjwa wa Saratani. Hii ni kwa sababu kusomea huu ungonjwa wa Saratani unachukuwa muda mrefu na fedha nyingi sana. Daktari akimaliza kusoma, hawezi kuja kufanya kazi kwa hospitali zetu za kitaifa ama kaunti kwa sababu hawalipi vizuri. Serikali Kuu na zile za kaunti zimeweka fedha kwenye miradi mingine na afya haipewi kipao mbele. Hii ndio kwa sababu sasa hivi Serikali imepea Building BridgesInitiative (BBI) kipao mbele badala ya madaktari ili waweze kuhudumia wagonjwa wetu kwenye hospitali. Nitamalizia kwa kusema kwamba Mungu amlaze Mhe. Waititu mahali pema peponi. Asante, Bw. Spika."
}