GET /api/v0.1/hansard/entries/1049896/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1049896,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1049896/?format=api",
    "text_counter": 102,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika. Kule nyumbani watu wanasema mshale ukiingia nguruwe huwa uko tamu kuliko ukiingia wewe binadamu. Hii inamaanisha kwamba hushughuliki yakitokea kwa mwingine, lakini yakitokea kwako inakuwa jambo la kusikitisha. Taarifa hii iliyoletwa na dada yetu, Sen. Were, ni Taarifa ya kuhuzunisha sana. Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba tunaweza kuruhusu watu kutoka nchi za ng‟ambo, wazungu, na wengineo ambao wako na nia ya kuja kuanza biashara kama hizi Kenya. Wakati wanaanza hizi biashara inakuwa rahisi sana. Wanaweza kuanza hizi nyumba za kuweka watoto yatima, na hatimaye wanachukua watoto wadogo sana na kuwaweka katika zile nyumba. Bw. Spika, makosa ambayo yanafanyika hapa ni kwamba katika hizi nyumba hakuna uchunguzi unafanywa na serikali zetu za mashinani. Vile vile, hakuna uchunzguzi unafanywa na Serikali yetu ya kitaifa kuona ya kwamba mtu akipewa ruhusa ya kuanza biashara kama hio ama usaidizi kama huo, anafaa kuchunguzwa kwa kina ijulikane kule alikotoka, alikua anafanya nini, na anataka kufanya nini hapa. Kunafaa kuwe na mkataba maalumu kuliko kuachiliwa hivi hivi. Ninakubaliana kwamba haya yametokea leo huko Bomet, lakini pia mambo kama haya yanatokea sana katika Mkoa wa Pwani. Watoto wadogo wanachukuliwa na wazungu, wanawekwa katika nyumba ikisemekana kwamba wanafanyiwa msaada na hatimaye wanabakwa wakiwa umri mdogo sana. Kwa sababu ya uwoga, hawawezi kusema, lakini kesi kama hizi zinatokea kila siku katika Mkoa wa Pwani. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}