GET /api/v0.1/hansard/entries/1050225/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1050225,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1050225/?format=api",
    "text_counter": 117,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Shukrani,Bw. Spika. Nimesimama kuambatana na Kanuni ya Kudumu No.48(1), kuomba Kauli kutoka kwa Kamati ya Usalama wa Taifa, Ulinzi na Mahusiano ya Kimataifa kuhusu ukatili wa maofisa wa kituo cha polisi cha Bamba kilichomo eneo Bunge la Ganze. Kauli inahusu kupigwa kwa mfanyibiashara maarufu Mama Kadzo Karisa Kalu mbele ya wafanyikazi wake na mali yake kuharibiwa. Bw. Spika, katika Kauli hiyo, Kamati ya Usalama wa Ndani inapaswa kueleza: (1) Sababu za ukatili wa polisi wa Kituo cha Bamba katika eneo Bungle la Ganze, ambao ulisababisha kupigwa kwa mama Kadzo Karisa Kalu na kuharibiwa kwa mali yake. (2) Ni lini mama Kadzo Karisa Kalu ataregeshewa mali yake ambayo ilishikwa na hao polisi, ili kuruhusiwa kuendelea na biashara hiyo. (3) Ni kwa nini au ni hatua gani zimechukuliwa na Serikali kuadhibu hao polisi waliofanya kitendo hicho cha ukatili ama unyama kwa kuharibu mali ya mama Kadzo Karisa Kalu. (4) Hiyo Kamati iweze kufafanua kimasomaso, ni kwa nini polisi wa Kituo cha Bamba wamezembea kazini wakinyanyasa wakaazi wa eneo la Bamba kwa kuwashika ovyo na kuomba hongo, badala ya kudumisha hali ya usalama wa Bamba? (5) Ni kwa nini waliohudumu kwenye Kituo hicho zaidi ya miaka mitatu au mitano, huo ni muda mrefu na mpaka sasa hawajapewa transfer au kuhamishwa kutoka Kituo cha Bamba? (6) Ikiwa wamezembea kazini, ni kwa nini Serikali haijachukuwa hatua ya kuwafurusha kutoka kwa hiyo kazi. Asante."
}