GET /api/v0.1/hansard/entries/1050226/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1050226,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1050226/?format=api",
    "text_counter": 118,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Zani",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13119,
        "legal_name": "Agnes Zani",
        "slug": "agnes-zani"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika. Kwanza ningependa kushukuru kwamba sasa katika Seneti tunampangilio wa orodha ambao umeandikwa kwa lugha ya Kiswahili. Nafikiri vile ambavyo tunaendelea na Kanuni za Kudumu za Seneti, pia tutaendelea kutumia Kiswahili zaidi tukizungumza katika Seneti. Kwa wakaaji wa Kilifi, kwanza ni kusema pole na kumshukuru Sen. Madzayo kwa kuleta mambo haya, ili Seneti ijue ya kwamba katika eneo la Bamba, mwanamke ambaye ni mfanya biashara, ambaye anafanya kazi yake wakati huu ambao pia biashara ni duni ameng’ang’ana na amepigwa, na bidhaa zake kuchukuliwa. Mali yake imechukuliwa na haijarejeshwa kwake. Hili ni jambo la kutatanisha sana. Nafikiri yale maombi ambayo Sen. Madzayo ameyasema hapa yanafaa kuangaliwa. Kwanza katika kituo cha polisi ambacho kiko Bamba, mambo kama hayo yaweza kuendelea vipi na mtu yeyote asiseme chochote na wale polisi wasiulizwe jambo lolote ? Kwa hivyo, Kamati ya Usalama wa Taifa, Ulinzi na Mahusiano ya Kimataifa lazima iangalie jambo hili. Pengine hata ni ukora umefanywa, kwa sababu, ukichukuwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}