GET /api/v0.1/hansard/entries/1050229/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1050229,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1050229/?format=api",
    "text_counter": 121,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kwamboka",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 9246,
        "legal_name": "Beatrice Kwamboka Makori",
        "slug": "beatrice-kwamboka-makori"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika. Ningependa kuunga mkono Sen. Madzayo kwa kuleta Taarifa hii katika Seneti. Kwa hakika, ni aibu sana kuona askari wakimpiga mama. Hiyo ni aibu kubwa sana kwa sababu akina mama wanafaa waheshimiwe. Hakuna mama ambaye anatarajiwa kupigwa na polisi. Ni tabia mbaya sana kuona askari wakiomba hongo kutoka kwa raia. Hiyo ni tabia mbaya sana na wanafaa wafunzwe adabu na sheria inafaa ichukuliwe. Ninashukuru kwa sababu niko kwenye Kamati ya Usalama wa Kitaifa, Ulinzi na Mahusiano ya Kigeni. Kwa kweli, tutachangia vilivyo na tutahakikisha kuwa mama Karisa amepata haki yake."
}