GET /api/v0.1/hansard/entries/1050245/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1050245,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1050245/?format=api",
    "text_counter": 137,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Bi. Naibu Spika, jambo kama hili limetendeka tena kwa upande wa Jacklyn Mugure. Hii ni tabia ya kuzembea kazini kwa askari wetu. Sasa imefika wakati Wizara ya Bw. Matiang’I, ambayo inahusika na mambo ya polisi na jinsi wanavyoweka bunduki zao, ingekua vyema kama mtu hajaelewa kutumia bastola asipewe bastola ya kuenda kwa wananchi kisha anawaumiza. Jambo kama hili linatokea sana katika Kaunti ya Kilifi. Kila siku kule Kilifi hakukosi vijana, wazee au watu ambao wanafukuzwa na polisi. Ikifika usiku, watu wanashika roho zao ndani ya mikono kwa sababu hawaezi kutembea bila kuwa free ilhali hii Kenya ni nchi yetu. Tunasema kwamba wakati umefika sasa hususan huyu Jacklyn Mugure uchunguzi wa kutosha ufanywe na askari aliyepiga risasi huyu mama na kumuua achukuliwe hatua kali. Asante."
}