GET /api/v0.1/hansard/entries/1050510/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1050510,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1050510/?format=api",
"text_counter": 73,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kieni, JP",
"speaker_title": "Hon. Kanini Kega",
"speaker": {
"id": 1813,
"legal_name": "James Mathenge Kanini Kega",
"slug": "james-mathenge-kanini-kega"
},
"content": " Ahsante, Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii nitoe risala za rambirambi kwa jamaa na marafiki wa rafiki yangu Mhe. Waititu. Wingu la simanzi limetanda katika taifa letu na kule Juja kwa sababu tumempoteza Mbunge na pia rafiki yetu. Nilijuana na Mhe. Waititu mwaka wa 2013 tulipokuwa tunafanya kampeni. Wetu ulikuwa ni urafiki wa mara ya kwanza kwa sababu yeye ni mcheshi na mpenda watu. Kama walivyosema Wabunge wenzangu, jina ‘Wakapee’ linatokana na ule moyo wake wakupeana. Tulipokuwa na yeye hapa Bunge, mara nyingi, tulipokuwa tunakunywa naye chai, hakuwa anapatia mtu nafasi ya kulipa. Pili, kinyume na Wabunge wengi ambao hawaishi katika maeneo bunge ambayo wanawakilisha, Mhe. Wakapee alikuwa anaishi Juja. Kila wakati ukienda huko, ulikuwa unapata akijiendesha na kukaa na wananchii. Labda, hiyo ndio sababu waliweza kumpatia nafasi ya pili kuwahudumia kama Mbunge wao. La mwisho, nilikuwa mmoja wa wale walienda nyumbani kwake alipokuwa anaugua. Kila wakati tulipoenda kumtembelea, alikuwa anauliza: “Ile Bill yangu imefika wapi?” Hata kama alikuwa anaugua sana. Kwa hivyo, ni vizuri Mhe. Duale amesema kuwa atachukua Mswada huo. Kama kuna kitu kizuri tunaeza patia familia ya mwendazake Mhe. Wakapee ni kuhakisha kwamba tumeleta Mswada huo na tumeukamilisha. Ugonjwa huu wa saratani umekita mizizi katika kila familia. Hakuna familia moja katika Bunge hili ambayo inaweza kuwa haijaathiriwa na ugonjwa huu. Tunajua kuwa ugonjwa huu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}