GET /api/v0.1/hansard/entries/1050513/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1050513,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1050513/?format=api",
    "text_counter": 76,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taita Taveta CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Haika Mizighi",
    "speaker": {
        "id": 13274,
        "legal_name": "Lydia Haika Mnene Mizighi",
        "slug": "lydia-haika-mnene-mizighi"
    },
    "content": " Ahsante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii. Kwa niaba yangu na ile ya watu wa Taita Taveta ninaowaakilisha hapa Bungeni, naleta rambirambi zangu kwa watu wa Juja na hata familia ya Mhe. Waititu, almaharufu, Wakapee. Nataka kumwomboleza mheshimiwa huyu kama kiongozi shujaa sana. Alikuwa mpole na mpenda watu. Kipindi kidogo nilichojuana na yeye, nilimwona kama mtu aliyekuwa na upendo sana. Nilimfahamu pia alipokuwa anafanya uhamasisho wa mambo haya ya saratani. Mara kwa mara, tukipata fursa ya kukaa na yeye, alituongelesha na kutueleza umuhimu wa kuzingatia afya zetu kwa kwenda kupata uchunguzi wa kimatibabu. Alitupatia historia ya alivyopata kujua kuwa anaugua ugonjwa huu wa saratani. Kwa hivyo, tunamwomboleza kama shujaa aliyepigana vita na ugonjwa huu wa saratani, na alikuwa na matumaini makubwa ya kushinda vita hivyo. Tulikuwa tunakutana na Mhe. Wakapee katika ibada zetu za misa za Wakatoliki hapa Bungeni. Kama Wakatoliki, kipindi hiki cha Kwaresma ni kipindi cha kusali, kufunga na kutoa. Kama Wakatoliki, tutamwombea sana Mungu aipatie familia yake faraja. Eh Bwana, umpe, eh Bwana, na Mwanga wa milele umwangazie milele ili apumzike kwa amani. Amina. Ahsante sana, Bw. Spika."
}