GET /api/v0.1/hansard/entries/1051162/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1051162,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1051162/?format=api",
    "text_counter": 44,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Omanga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13175,
        "legal_name": "Millicent Omanga",
        "slug": "millicent-omanga"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika. Kwanza ningependa kutoa rambirambi zangu kutoka kwa familia yangu na watu wa Nairobi kwa jumla. Tunasema pole kwa watu wa Kiambu, hasa Juja. Mhe. Waititu ni mtu ambaye ungemuita hustler. Umesikia Seneta wake akisema kwamba alianza kama kijana wa mkono lakini akafanya kazi kwa bidii hadi akawa meneja. Alifanya biashara kwa bidii hadi akawa Mbunge wa Juja kwa muhula wa pili. Niliweza kumjua Mhe. Waititu wakati tulifanya kazi pamoja katika ile vuguvugu ambayo wengi wanaiita „Tangatanga‟, „ hustler’ au „kazi ni kazi.‟ Pale ndipo niliweza kumjua kama mtu mjakazi sana. Mhe. Waititu alikua anapenda kazi yake na mtu jasiri aliyetetea watu wake wa Juja. Alipenda maendeleo. Ni huzuni sana kwamba tumempoteza Mhe. Waititu kwa sababu ya ugonjwa wa saratani. Nimesikia viongozi wengi wakilalamika na kusema kuwa Kamati ya Afya haifanyi hili au lile. Kuna mambo ambayo Kamati ya Afya haiwezi kufanya na mambo mengine ambayo Seneti au Wabunge tunafaa kufanya kwa jumla. Bw. Spika, miezi mitano ama sita hivi iliyopita tulileta Mswada hapa kama Kamati Maalum ya Managed Equipment Service (MES ). Kulikuwa na maoni mazuri kwenye hiyo Ripoti. Tulionyesha vile pesa zinavujwa kwenye Wizara ya Afya. Lakini kulifanyikaje? Viongozi wa Bunge hili la Seneti waliwashawishi Maseneta kupiga kura kulingana na mwongozo wao wa siasa. Hata Kamati ikiandika ripoti, ikija hapa Seneti, ni vile vigogo wetu wa siasa watasema tupige kura ndivyo tutapiga. Tumeona kwa Miswada nyingi kama ile ya"
}