GET /api/v0.1/hansard/entries/1051221/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1051221,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1051221/?format=api",
    "text_counter": 103,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Bw. Spika, jambo dhaifu zaidi upande wetu ni korti zetu. Kitendo kama hiki kikitokea, kikiripotiwa, mtu anashikwa na kupelekwa kortini, halafu korti inaangalia inamuachilia. Ninampongeza sana Bii Ruto ambaye alichukua hii kesi kwa hasira na hatimaye akaipeleka kwa korti za ng‟ambo na sasa hukumu imepatikana. Yule mtu aliyefanya kitendo hicho kwa wale wasichana wadogo wa Kenya amefungwa miaka mingi. Lazima korti zetu hapa Kenya ziige mfano kama huu ya kwamba watu ambao wanabaka watoto wadogo wasiachiliwe hata kidogo. Wakati mwingine yule dada yetu Naomi akisema mambo haya yanafanywa namna hii, inaonekana ni kama tunaweza kuunga mkono. Huwezi kufikiria jinsi mtu baro baro, mzima wa miaka arubaini na kitu analala na mtoto wa miaka mitatu ama sita. Unaenda wapi sasa na mtoto ambaye hata hajakuwa mwanamke ambaye unaweza kulala naye?"
}