GET /api/v0.1/hansard/entries/1051552/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1051552,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1051552/?format=api",
    "text_counter": 115,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": " Asante Naibu Spika wa Mda kwa kunipatia hii nafasi. Ni muhimu sana tuwe na hizi maktaba. Zitatusaidia kuwa na uzoefu au desturi ya kusoma na kutuepusha na mambo mengi ya ushetani. Wakati unaoutumia katika maktaba unaweza kukupunguzia mambo mengi, zaidi kwa wale vijana tuko nao. Lakini zikitengenezwa, ziwe maktaba na sio jina; ziwe maktaba za kiwango cha hali ya juu. Maktaba hizo ziwe na mambo mengi. Hata kompyuta zinafaa kuwa hapo ndani. Hizi maktaba zikiwa, zitatusaidia sana sisi watu wa Lamu maanake katika youth walioharibika zaidi ni kwetu Lamu. Vijana wameingia kwenye mihadarati. Ukienda ukiona watoto wetu, wanasinzia. Kwa hivyo, ikipatikana njia yoyote kama hii itasaidia wale watoto wetu. Ni mambo ya kusikitisha. Tunang’ang’ana lakini bado kuna haja ya kung’ang’ana zaidi. Chochote kinachopangwa kwenye Serikali isiwe kupangwa vile inavyopangwa kwamba kila eneo-bunge lipate maktaba moja. Tukumbuke mazingira na maeneo Mwenyezi Mungu alivyotuumba. Watu wanafaa waende wakatuangalie sisi kule Lamu maanake sehemu nyingi ni visiwa. Ikisemekana sisi tuna maeneo-bunge mawili na ziwekwe maktaba mbili, pia yanakuwa matatizo. Mtu akitoka Kiunga, tuseme aje Kisiwa cha Pate, ni Ksh2,000. Kwa hivyo haitatusaidia. Sasa zile sheria zinazopangwa zipangwe sawasawa. Tuseme, kama hapa Nairobi kuna maeneo- bunge kumi na saba. Kwao ni sawa kila eneo-bunge likipata maktaba. Lakini sisi tuna maeneo- bunge mawili lakini hata maktaba kumi hazitutoshi maanake ukimtoa mtu Msitu wa Boni umuambie aje Kisiwa cha Pate, hakuna usafiri wa kawaida. Usafiri ni lazima uchukue wako, ukodishe boti uende. Hivyo ni lazima tujuane na tuelewane na tuwaelewe watu wengine kwamba maeneo Mungu aliyowaumbia ni tofauti. Lakini hatulalamiki kwamba yale maeneo ni magumu. Hapana. Ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ameyaumba vile. Kuna manufaa mengine tumepata. Kama kwetu, mradi wa LAPSSET haungeweza kutengezwa Nairobi. Ni lazima utengezwe Lamu kwa sababu sisi tuna bahari. Pia, tukipata hizi rasilimali tusiwe tutajifikiria sisi. Kama mfano, Nairobi na Mombasa ni tofauti. Pia, Lamu iko hivyo. Tutembee tuone zile sehemu ziko vipi ndio sote tujihisi Wakenya."
}