GET /api/v0.1/hansard/entries/1051713/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1051713,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1051713/?format=api",
    "text_counter": 113,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Trans Nzoia CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Janet Nangabo",
    "speaker": {
        "id": 1076,
        "legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
        "slug": "janet-nangabo-wanyama"
    },
    "content": " Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nichangia Mswada huu wa maktaba katika nchi yetu ya Kenya. Vile wanenaji waliotangulia wamesema, ni muhimu tuwe na maktaba katika nchi yetu ya Kenya. Ni kweli watoto wetu wameharibika kwa sababu hawajapata nafasi ya kuenda kusoma katika maktaba mahali popote. Wengi wamerudi kuvuta bangi. Wengine wamerudi kwenda tu kunywa pombe. Nilitembea ng’ambo kule England na nikaingia katika maktaba katika nchi hiyo na nikaona kwamba iko na vifaa ama vitabu vile vinatosha kabisa kusema hata historia katika nchi hiyo na hata historia ya viongozi katika nchi hiyo. Ndiposa, kama sisi pia tutapitisha Mswada huu, itakuwa vyema kwetu kwa sababu watoto na hata wazee wetu hawataumia. Ukiona katika nchi yetu ya Kenya saa hii, kila mtu ama mtoto anataka achukue kitu nyumbani auze ndiposa awe na simu ya rununu. Vile Mhe. (Dkt) Shaban amesema, hawa watoto hawatumii simu hizi kwa njia iliyo bora. Wanazichukua na kuangalia picha zisizo na mambo sahihi. Vile wanasema kwamba maktaba hii ni ya kitaifa, ninaona ni vyema na ni heri pia tuwe nazo nyumbani. Vile umesema kwamba tuko na moja yao katika Nairobi hapa, unaona kwamba hao watoto ama watu kutoka kule sehemu za nyumbani hawatapata nafasi ya kuangalia kwamba hii maktaba iliyo huku kwa kitaifa iko namna gani. Ni vyema tuwe nazo kule chini. Hata sisi kama viongozi tutatumia hiyo nafasi kuhamasisha watu na kusema kwamba tukitaka kuwa wasomi wazuri na tukitaka hata kufanya kazi nzuri ama tukitaka kusema kwamba huenda mtu ana kipawa cha kufanya kitu fulani, itakuwa ni vyema kwamba ameenda katika hiyo maktaba na amehakikisha kwamba amepata ujuzi ama anasoma vizuri ndiposa atakuwa anaelewa kitu. Vile wamesema kuhusu hii maktaba, ni vyema kwa sababu imeweka kila mtu katika nafasi hiyo. Ni vizuri kwa sababu watakuwa ni watu wale wamehitimu na watakuwa wanasaidia katika hizo maktaba kuhakikisha kwamba watu wanaoenda katika maktaba hiyo wanapata nafasi nzuri ya kusoma na kuelewa ni nini wanasoma. Shida yangu ni utekelezaji wa hii Miswada tunapitisha katika Bunge letu. Unaona kwamba inachukua muda mno kuhakikisha kwamba imetekelezwa. Iwapo itatekelezwa, nafikiria itakuwa ni nafuu kwetu sisi viongozi na hata kule nyumbani na kwa wale watu tunawakilisha. Nakumbuka nikiwa katika shule ya upili, tulikuwa na hizi maktaba. Lakini unaona kwamba zilikuwa na vitabu hivyo vya historia, ama ukifanya mambo ya lugha, inakupata unasoma hiyo katika maktaba hizo lakini hatukuwa na vitabu vya kutosha enzi zile. Iwapo tutakuwa nazo kama wakati huu, wengi tutakuwa tunafahamu na inatusaidia kujua mambo mengi katika jamii zetu na hata katika mienendo yetu. Ninasema asante na ninaunga mjadala huu mkono."
}