GET /api/v0.1/hansard/entries/1051953/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1051953,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1051953/?format=api",
"text_counter": 190,
"type": "speech",
"speaker_name": "The Temporary Speaker",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "(Sen. (Dr.) Mwaura): Asante sana, kwa umahiri na ushupavu ambao umezungemza nao Sen. Orengo, kiongozi wa Wachache. Umetukumbusha mambo ya kule Gbadolite Mobutu Sese Seko. Kuna hekima nyingi zatokea hapa katika Ukumbi huu wa majidiliano na malumbano lakini uamuzi ndio wa maana hususan, tukiangazia mirengo ya kisiasa na pia matazamio ya waka kesho. Hapo ndio kuna kasheshe kidogo kwa sababu sisi kama viongozi tumependekeza wajibu wetu wa kufanya maamuzi yaliyo bora kwa nchi yetu. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Bajeti, sijui kama ni Waziri Butu wa Hazina, karibu Sen. (Eng) Mahamud. Ulifukuzwa na mimi nikafukuzwa kwa mtawalia. Una nafasi ya kuzungumza."
}