HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1052192,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1052192/?format=api",
"text_counter": 193,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": "Kwanza, nampongeza kwa kuja na Mswada huu mzuri ambao tumeona una faida tele. Vile vile, nampongeza Mkuu wa Chama Kikuu Mheshimiwa Amos Kimunya ambaye alikuwa ni Waziri wa Ardhi wa zamani kwa kutufafanulia vizuri sana juu ya maswala haya . Kwa hivyo, nikiangalia mzungumzaji mwenzangu Mheshimiwa Denittah Ghati, ameeleza na akasema walienda hata huko Mombasa. Nataka kusema kuwa swala la ardhi likiongolewa wakati wowote, sisi tuliyoko katika maeneo ya Pwani ndio watu ambao tumeathirika zaidi. Tukiangalia, tunaona katika Mswada huu mahali ambapo panawekwa kuwa ni ardhi ya umma, hasa katika ugawanyaji wa ardhi. Tunajua kuwa watu kupata vyeti vya mashamba ni lazima waweke majumba yanayoshughulikia maswala ya kijamii kama makanisa, misikiti, shule, hospitali na mangine. Nataka kuungana mkono na Mhe. Amos Kimunya kusema kuwa wakati wa ugawaji wa ardhi, kitu cha kwanza kabla hujapeana cheti, katika vile vipande vingine, hivi vipande vya shule, hospitali ama makanisa, ni mwanzo vipewe hati miliki kabla ya wale wengine kupewa. Jambo hili limetupa shida sana. Ukiangalia mahali kama eneo langu la Bunge la Jomvu, kuna mahali wananchi wamekaa kwa muda mrefu sana katika sehemu za Ganahola, Bangaladesh, Kibarani na sehemu zingine. Wananchi wenyewe wanatoa ardhi wakitaka shule ijengwe hapo na pesa za National Government Constituencies Development Fund, lakini unaona shida ni kuwa ufikapo kwa bodi, hapo huna makaratasi ya hati miliki . Kwa hivyo, inabidi uanze kuenda kwenye mpangilio mrefu sana wa kuweka mikutano na vile vile kupata vyombo vya Serikali kuthibitisha kama hapo mahali kweli panatakikana shule, kanisa, hospitali ama msikiti. Naona kuwa tukiangalia shule kwa kuwa hii ni shida kubwa sana... Kule Mombasa, shule zote hazina vyeti miliki vya mashamba, ilhali zimekuwa pale tangu tulipopata Uhuru. Kupitia Mswada huu, nina hakika kuwa shule zote zitapata vyeti miliki na kuweza kujisaidia.Tukiangalia hati miliki, ina faida kubwa sana kwa sababu ukiwa nayo, unaweza kwenda benki na kupata pesa na ikakusaidia. Kwa hivyo, pia katika hizo shule, wakipata hati miliki, wakati mwingine wanapata pesa kutoka kwa Serikali kupitia Wizara ya Elimu. Wanapata pesa kupitia kwa vyama vya wazazi na waalimu au kwa mambo yao ya shule. Pia, watakuwa na uwezo wa kuchukua hati miliki na kupeleka benki na kuendeleza mambo yao ya shule. Vile vile, mambo haya yataweza kutusaidia sana kupunguza mambo ya uporaji wa mashamba. Hii ni kwa sababu kuna watu katika dunia hii, wakiona ardhi ya umma, wanadondokwa na mate. Wanafikiria tu ni jinsi gani wataiba ardhi ile. Ukifuatilia, watakuambia ardhi ilikuwa tangu wakati wa mitume na haijakwisha hadi leo, sisi ndio tutamaliza? Hao ni watu wabaya na wafisadi. Lakini tukiangalia mambo kama haya, yataweza kusaidia kuona kuwa zile ardhi ambazo zimewekwa kwa ajili ya umma, hazitaweza kuvamiwa na kuchukuliwa. Nazungumza haya kwa ajili ya mfano ambao niko nao. Mwaka 2007, nilikuwa Diwani kabla ya kuwa Mbunge. Wakati huo, kuna hospitali inaitwa Mugusi ambayo tulipigania sana kuona kuwa inahudumia wananchi. Lakini baada ya muda fulani kidogo, tukaona kuwa kipande cha ardhi hicho kimekatwa na kimejengwa nyumba za ghorofa. Kiliachwa kipande nusu na ndicho ambacho kinatumika katika mambo ya hospitali. Hivyo basi, mimi nikiwa Mbunge, nataka kusema kuwa jambo hili limekuwa ni la kutufungua macho kupitia kwa Mswada huu. Mambo kama haya hayataendelea katika jamii zetu; mambo ambayo yametajwa hapa na Mheshimiwa Kimunya kama ya Shule ya Msingi ya Lang’ata na sehemu nyinginezo. Leo tukiwa Wajumbe, imetubidi sasa tuweke pesa sana kwa kujenga ua za kuta katika zile shule. Wakati huu wa COVID-19 ambao ni wakati mgumu sana, watoto hawana madarasa. Lakini kwa ajili ya kuogopa ardhi ya shule iibiwe, twaweka hizo pesa kwa kujenga vikuta badala ya pesa hizo zitumike kujenga madarasa katika hizo shule. Kwa hivyo, ukija The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}