GET /api/v0.1/hansard/entries/1052193/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1052193,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1052193/?format=api",
    "text_counter": 194,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": {
        "id": 1612,
        "legal_name": "Bady Twalib Bady",
        "slug": "bady-twalib-bady"
    },
    "content": "Mswada huu kwa upande wa sheria, itakuwa hamna haja ya kupata shida sana kuweka pesa zile kwa sababu kila ardhi itakuwa inajulikana kipimo chake kinatoka mahali gani mpaka wapi. Kwa hivyo, jambo muhimu ambalo mimi nauliza ni hili: Kando na Mswada huu, Wizara ya Ardhi iende na nguvu sana na ihakikishe shule zetu zote na hospitali zimepewa hati miliki za ardhi. Vile vile, nachukua fursa hii kusema kuwa mimi katika Eneo Bunge la Jomvu, tumejaribu sana tangu wakati wa Mhe. Muhammed Swazuri, tumempeleka katika sehemu 32 ambazo zilifaa zipewe hati miliki za ardhi. Lakini mpaka saa hizi, ni sehemu nne peke yake ambazo tunaanza kuzifanyia kazi. Tukiangalia sehemu ya Mikanjuni, tumepata hati milki 639. Nashukuru Serikali ya Kaunti ya Mombasa kupitia Mhe. Ali Hassan Joho ambaye atakuwa Rais wetu wa tano kulingana na sisi watu wa Pwani. Kwa hivyo, kupitia huu mpangilio wa Benki Kuu ya Ulimwengu, tumeona kwamba ameweza kutoa hati miliki za seheme za Misufini na Kwakya Kwa Thome ambazo ziko tayari. Juzi, tumeona hati miliki za Kisumu Ndogo zimetoka."
}