GET /api/v0.1/hansard/entries/1052245/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1052245,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1052245/?format=api",
"text_counter": 246,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kassim Tandaza",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13287,
"legal_name": "Kassim Sawa Tandaza",
"slug": "kassim-sawa-tandaza"
},
"content": "Kassim (Matuga, ANC): Asante sana, Bw. Mnenaji kwa sababu katika Kiswahili sanifu, Spika anaitwa mnenaji. Kwanza, natoa pongezi kwa Mhe. King’ara kwa kuleta Mswada huu ambao utaweza kusawazisha donda sugu hasa kwa mimi Mbunge wa Matuga. Ni wiki iliyopita tu ambapo niliitwa katika shule moja inayoitwa Bombo pale Kiteje. Kuna bwenyenye mmoja ambaye alikuwa ameweka ua kwenye afisi ya mwalimu mkuu akidai kuwa iko kwenye shamba lake. Hii ni shule ambayo imekuwa pale kwa zaidi ya miaka 30. Hali kadhalika, imenibidi kutoa pesa za National Government-Constituency Development"
}