GET /api/v0.1/hansard/entries/105323/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 105323,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/105323/?format=api",
"text_counter": 208,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Kutuny",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 61,
"legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
"slug": "joshua-kutuny"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, nataka kusema kwamba kwa mara ya kwanza, namshukuru Waziri Mkuu kwa kufafanua vizuri kwamba maswala ya Katiba yatakuwa kulingana na demokrasia na hisia ya yeyote katika taifa la Kenya. Ni wakati muhimu ambapo taifa la Kenya litatatua kitendawili ambacho kimekuwepo kwa zaidi ya miaka 20; kuwepo Katiba ama kusiwepo. Kwa sasa, inajulikana kwamba kuna vikundi viwili; âlaâ, na ândioâ. Tungependa sisi mrengo wa âlaâ Waziri Mkuu athibitishe madai kwamba Serikali imepeana onyo kali kwa vyombo vya habari na wahusika wa utoaji wa habari kwamba taarifa isikuwe sawa kwa wanaounga Katiba na wanaoipinga, kwa sababu kwa ripoti yao kwa sasa, inamaanisha kwamba wana mapendeleo. Wale wanaounga Katiba wanapewa nafasi ya kutosha kutoa madai yao na wale wanaosema âhapanaâ wanakatazwa nafasi ya kutosha ya kutetea maswala yao."
}