GET /api/v0.1/hansard/entries/1053374/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1053374,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1053374/?format=api",
    "text_counter": 142,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": " Ahsante, Mhe. Naibu Spika. Ningependa kutumia fursa hii kumpongeza Mhe. Kassim Tandaza kwa kuja na Mswada huu. Sote tunafahamu kwamba ukulima ndio uti wa mgongo katika maisha ya leo. Mumea huu, ambao Mhe. Kassim Tandaza ameutaja, ni mmea ambao unapatikana katika sehemu za Pwani, hususan katika maeneo ya Lamu na Kwale. Kabla sijazungumzia mumea huu, ningependa kuzungumzia swala nzima la ukulima na faida ya ukulima, hususan katika nchi hii na eneo la Pwani. Mbali na kuwa tunafahamu kwamba ukulima ndio muhimu sana katika uchumi wetu, tumeona wazi ya kwamba watu wanategemea ukulima katika mambo mengi. Kwa masikitiko makubwa, nikizungumzia eneo la Pwani, ukulima umefifia sana kwa sababu ya kutotiliwa nguvu na kutosaidiwa na Serikali. Ninaamini kwamba Wapwani wanapenda maswala ya ukulima na wanajitahidi sana. Lakini katika swala hili, Wapwani hawajasaidika na namna ya kujiendeleza na ukulima wao. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}