GET /api/v0.1/hansard/entries/1053375/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1053375,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1053375/?format=api",
    "text_counter": 143,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Kwa hivyo, Mhe. Naibu Spika, tunapojadili swala hili, ni vyema tufahamu na Serikali ijue ya kwamba Wapwani wanahitaji usaidizi katika kuendeleza ukulima. Kuwe kwamba tuko na ardhi za kutosha na mimea ya kutosha. Katika hali hii, tunaamini ya kwamba angalau tutapata misaada kama vile misaada mingine inavyotolewa katika sehemu nyingine katika nchi hii. Tukifanya hivyo, Pwani itakuwa na ukulima mwingi na wengi watajiingiza katika jambo hili ili waweze kusaidika na kusaidiwa kuliendeleza jambo hili. Ni vyema tufahamu kwamba katika hali ya uchumi wetu hivi sasa, ukulima ndio jambo ambalo tunahitaji kulipea kipaumbele. Ardhi tuko nazo na wanaohitaji kufanya ukulima tuko nao lakini Serikali lazima ijitokeze, kupitia kwa wizara husika, kuhakikisha ya kwamba wakulima hawa wamesaidiwa kwa njia zote wanazotaka na kuhamasishwa, ili kuhakikisha ya kwamba wameweza kufanya ukulima wao ili kujiendeleza na kujimudu katika maisha ya leo. Kwa haya, ni wajibu wa Serikali kuhakikisha wakulima wa sehemu zote wamefaidika, hususan Wapwani, nikiamini pakubwa kwamba wakulima wa Pwani wameachwa nyuma kwa kutosaidiwa na Serikali katika swala nzima la ukulima. Ahsante."
}