GET /api/v0.1/hansard/entries/1053450/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1053450,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1053450/?format=api",
    "text_counter": 218,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kaloleni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Paul Katana",
    "speaker": {
        "id": 13357,
        "legal_name": "Paul Kahindi Katana",
        "slug": "paul-kahindi-katana-2"
    },
    "content": "majimbo yetu ili wajue ni mumea upi waweza kutumika kuzalisha na kuleta mapatao katika maeneo haya na nchi kwa jumla. Kwa muda mrefu, mimea kama kahawa, chai, korosho, na mnazi ilikuwa ikisifika kwa mazao yake lakini, kwa sasa mimea hii imefifia. Tunajua kwamba kilimo ni uti wa mgongo wa nchi hii. Serikali inatakikana kuweka bajeti kubwa kwa Wizara ya Kilimo ili utafiti ufanywe wa kusaidia wakulima wa mimea hii. Kule Pwani, tuko na mimea ya mnazi mkorosho na Bixa. Mimea hii imekua ikileta mapato lakini, tangu viwanda vya mkorosho na Bixa vifungwe, hali ya uchumi wa jimbo la Pwani imerudi nyuma. Ni jambo la aibu kuwa kwa sasa tunaagiza tui la nazi kutoka nchi ya Malaysia ilihali Pwani tuna mumea huu ambao unaweza kutumika kutoa zao hilo. Vile vile, kama Serikali inaweza kufanya utafiti wa mimea hii mitatu Pwani, inaweza kutoa suluhu la ukosefu wa ajira katika jimbo la Pwani na kenya nzima. Kwa muda mrefu, ifikapo wakati wa uchaguzi, watu wengi huja Pwani na kuwahadaa Wapwani kwamba watawekeza kwa mnazi na kufufua viwanda vya mkorosho na Bixa lakini, ukienda kule baada ya uchaguzi, mimea hii haitambuliki. Nataka kuunga mkono Mswada huu. Bixa, mkorosho na nazi ziletwe katika ibara ya kwanza ya mimea ambayo inaweza kutumika kuzalisha na kuleta mapato katika taifa letu. Mnazi peke yake unaweza kuajiri zaidi ya watu elfu kumi. Kwa muda mrefu, watu wamekuwa wakiongea kuhusu bidhaa moja ya mnazi ambayo ni pombe peke yake. Mnazi una zaidi ya bidhaa kumi na moja. Kwa mfano, fuvu la nazi linaweza kutumika kutengeneza vifungo. Kwa sababu kilimo kimegatuliwa, serikali za kaunti zinaweza kuleta mitambo na kuajiri vijana wengi, ili waweze kujikimu kuliko kuwapa slasha wafyeke na kusafisha mitaro ya maji-taka. Pesa zinazotumika kule zinaweza kutumika kuwekeza kwa kilimo. Mhe. Naibu Spika, kama waweza kukumbuka, mti wa mnazi katika nchi ya Malaysia umefanya nchi hiyo kukua kiuchumi. Serikali haijafanya utafiti muhimu wa kuhakikisha kwamba mti huu unaweza kutupatia pato. Wakati huu wa ugonjwa wa COVID-19, ni kilimo peke yake ambacho kimeweza kusaidia wananchi kujikimu kimaisha. Naunga mkono Bixa kuletwa kwa ibara ya kwanza ya mimea. Vile vile, mnazi na korosho ziwekwe katika ibara ya kwanza ili tupate pesa ya kufanya utafiti na kutafuta masoko nchini na nchi za kigeni. Naunga mkono Mswada huu wa mabadiliko. Ahsante."
}