GET /api/v0.1/hansard/entries/1053452/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1053452,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1053452/?format=api",
"text_counter": 220,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taveta, JP",
"speaker_title": "Hon. (Dr.) Naomi Shaban",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": " Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hi. Mimi pia najiunga na wenzangu kumpongeza ndugu yetu mhe. Tandaza, Mbunge wa Matuga kwa kuleta Mswada huu ambao unarekebisha sheria za mimea hapa nchini. Kwanza, ningependa kutoa risala zangu za rambirambi kutoka kwangu pamoja na jamii yangu, Eneo Bunge la Taveta na Taita Taveta kwa ujumla kwa jamii za wabunge waliokufa. Bunge hili la Kumi na Mbili limepata kipigo cha kuwapoteza wabunge wengi. Tunawaombea na tunajua wametutangulia mbele ya haki. Kule walikokwenda, Mwenyezi Mungu aweke roho zao pahali pema peponi. Mti huu wa Bixa au mrangi kama unavyoitwa Pwani ni mti muhimu sana. Mbegu zake ni muhimu. Si bure tu Mhe. Tandaza amelivalia njuga jambo hili. Eneo lake haswa kule kwale ndiko kiwanda cha Bixa kiliko ambacho kinaweza kuhakikisha mumea huu wa Bixa unapatia watu faida. Ni sawa ikiwa mumea huu wa Bixa utaorodheshwa pamoja na mimea mingine muhimu hapa nchini. Si jambo la kutosha kuorodhesha tu. Orodha hizi zikitoka, mimea hii lazima ipatiwe kipaumbele. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}