GET /api/v0.1/hansard/entries/1053467/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1053467,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1053467/?format=api",
"text_counter": 235,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mbogo Ali (",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "nje. Kuna umuhimu mkubwa kwa Serikali kusaidia kuboresha mumea huu. Kama tulivyosema, ni lazima kwanza tuanze kwa kupitisha Mswada ulioletwa Bungeni na Mhe. Tandaza. Baada ya hapo, ni lazima sheria hiyo ipewe msukumo na nguvu na Serikali Kuu. Utafiti wa Bixa au mrangi uko chini. Sio huu mumea peke yake bali mimea mingi inayofanya vyema humu nchini imedidimia. Tulikuwa na vituo vya utafiti kama vile Kenya Agricultural Research Institute (KARI), ambavyo leo hii vimefungwa na hata ardhi imekuwa ikiuziwa watu wa kibinafsi. Tulikuwa na mashirika kama vile Agricultural Development Corporation (ADC) kule Pwani na kwingineko nchini. Mashirika hayo yalikuwa yakifanya utafiti ili kilimo kiweze kuimarika humu nchini. Leo hii hayo mashirika hayapo tena, hatujui yameenda wapi. Sisi kama Wapwani tunatambulika zaidi kwa mimea kama vile mnazi na mkorosho"
}