GET /api/v0.1/hansard/entries/1053469/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1053469,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1053469/?format=api",
    "text_counter": 237,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Mimea hii inatufanya sisi tutambulike kama Wapwani. Tulipokuwa wadogo, mkorosho ulikuwa unafanya vizuri sana katika eneo la Pwani. Tulikuwa na kiwanda kilichokuwa kikisimamiwa na Serikali Kuu kilichojulikana kama Kenya Cashewnuts Limited. Kiwanda hicho kilikuwa kimetoa motisha kwa wakulima wengi wadogo wadogo katika eneo la Pwani waliokuwa wakipanda mkorosho kwa wingi. Leo hii, ni jambo la kusikitisha na kutamausha kuona mkorosho umesahaulika na umekufa. Hii ni kwa sababu kile kiwanda muhimu tulichokuwa tukitegemea hakifanyi kazi tena. Jambo la kushangaza ni kwamba baada ya kiwanda kile kuanguka kule Pwani, kilifufuka kule Thika. Leo hii korosho kutoka Pwani hununuliwa na middlemen ambao huenda kuziuza kwenye kiwanda ambacho kiko mjini Thika kinachojulikana kama Afrimac Nut Company. Hili ni jambo la kusikitisha. Kiwanda cha mkorosho kilikuwa Pwani, na watu wa huko walikulia. Leo hii mkulima anaingia gharama kubwa. Korosho zetu zimekuwa ghali mno kwa sababu ya usafiri mrefu. Kuhusu mumea mnazi, tumeambiwa kwamba uko na faida zaidi ya kumi na moja. Mbali na faida kubwa inayojulikana, ambayo ni pombe ya mnazi, kuna mafuta ya nazi yanayojulikana kuwa tiba. Tumeambiwa na watafiti kwamba mafuta ya nazi yanatibu saratani. Kuna mnazi unaotoa makuti. Ukienda kwenye hoteli zetu za kifahari, utaona vile mapaa yao yameekezwa na makuti ambayo yanaonekana kuwa nadhifu na ya kupendeza. Ukiukata mnazi, unatoa mbao nyingi sana ambazo hutumika kwa ujenzi. Kwa hivo, mnazi uko na faida nyingi sana lakini ni mumea mmoja ambao umesahaulika na Serikali yetu. Hatujakuwa na hata kiwanda kidogo cha kushughulikia mumea wa mnazi. Kama tulivyoskia hapa, kilimo ndio uti wa mgongo wa Jamhuri ya Kenya. Tunajua kwamba kilimo huchangia asilimia 30 ya Bajeti ya Serikali Kuu. Pia tunajua kwamba kilimo kimeajiri zaidi ya asilimia 70 ya Wakenya, ambao hutegemea sekta hiyo kwa maisha yao ya kila siku. Jambo la kushangaza ni kwamba wakati tunaposoma Bajeti, au wakati mipango ya Serikali inapofanywa, kilimo huorodheshwa kama nambari kumi. Barabara, usalama na sekta nyingine chungu nzima zimepewa kipaumbele ilhali uti wa mgongo wa uchumi wa nchi hii, ambao tunajua unategemewa na asilimia 70 ya Wakenya, imeorodheshwa nambari kumi. Tunaiomba Kamati ya Bunge hili inayohusika na masuala ya kilimo iangalie jambo hili. Sisi ndio tunaopitisha Bajeti ya Serikali. Ni lazima tuamue. Kama tunafahamu umuhimu wa kilimo ni lazima, kama Bunge la Taifa, tuekeze zaidi kwenye sekta ya kilimo ili sekta hii iimarike irudi kama ilivyokuwa zamani. Tumezungumza mambo ya mabwawa au zile tunaita katika Kizungu ukiniruhusu dams . Serikali imewekeza zaidi katika kuhakikisha tumejenga madimbwi yale ili mvua itakapokuwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}