GET /api/v0.1/hansard/entries/1053470/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1053470,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1053470/?format=api",
    "text_counter": 238,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "imekuja, yale maji yasipotee bure. Sisi kama Wapwani tuna bahati kuu. Tuna mito miwili mikuu katika Jamhuri ya Kenya; Mto wa Tana ambao unaanzia milimani na unaishia Bahari ya Hindi. Tuko na Mto wa Athi River ambao unapitia maeneo ya Ukambani na unafika pale Sabaki na unateremka mpaka Bahari ya Hindi. Lakini wakati tumepata mvua ya kutosha, maji haya yote yanaishia katika Bahari ya Hindi. Lakini tukiweza kujenga vidimbwi hivi huko katikati, tunaweza tukachuma maji yale na yakatusaidia wakati wa ukame na tukahakikisha ukulima unakua katika maeneo mengi sana katika Jamhuri ya Kenya. Katika Pwani tumekuwa na mmea wa pamba. Tulikuwa na kiwanda kule Lamu kinajulikana kama Lamu Cotton Ginnery. Kiwanda kile pia kimekufa na kilikuwa kikipatiana mchango mkubwa sana kwa wakulima wadogo wadogo wa pamba kutoka maeneo ya Mpeketoni. Tumekuwa na kiwanda cha mkonge pale Vipingo Sisal. Kilikuwa kimeajiri zaidi ya watu elfu tano. Leo, kiwanda kile kimekufa na yale mashamba yote makubwa leo yamerudi mikononi mwa watu binafsi. Wanagawanya na kuuzia wananchi. Kwa hayo, naunga mkono Mswada huu. Asante sana."
}