GET /api/v0.1/hansard/entries/105349/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 105349,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/105349/?format=api",
"text_counter": 234,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Raila",
"speaker_title": "The Prime Minister",
"speaker": {
"id": 195,
"legal_name": "Raila Amolo Odinga",
"slug": "raila-odinga"
},
"content": " Bw. Naibu Spika, ninajibu swali ambalo liliulizwa kwa Lugha ya Kiswahili. Sichangii Hoja yoyote ila ninajibu swali. Kanuni zetu zinasema kama umeanza kuchangia Hoja au Mswada kwa Lugha ya Kiingereza, basi utaendelea hivyo hadi mwisho wa mchango wako. Kanuni hizi hazisemi lugha unayostahili kutumia ikiwa unajibu maswali tofauti tofauti. Kwa hivyo, nimeamua kumjibu hon. Kutuny kwa Lugha ya Kiswahili. Ningemuomba mhe. Kutuny awe na subira, maana yake sikuwa nimemaliza kumjibu kabla yeye kusimama kwa jambo la nidhamu. Subira huvuta heri. Ningependa kumwambia mhe. Kutuny kwamba Serikali haitaki kumtisha Mkenya wowote. Tumesema kuwa kila mtu atakuwa na fursa ya kufanya kampeni vile anavyotaka. Hatujatoa amri yoyote kwa vyombo vya habari eti wasitangaze maneno fulani na fulani. Katika nchi yetu, vyombo vingi vya habari ni vya watu binafsi na wala si vya Serikali. Kwa hivyo, wao wenyewe wana haki ya kutangaza maneno yoyote ambayo wanayataka. Ikiwa mheshimiwa anasema maneno ambayo vyombo vya habari vinaona hayana maana, wao wenyewe ndio watabagua au kuamua. Sio Serikali kufanya hivyo. Ningependa vile vile kumueleza mheshimiwa kuwa Serikali imejaribu kuwahimiza Wakenya wote wajiepushe na propaganda ambayo haina msingi. Kwa mfano, wengine wanasema Serikali itatenga ward maalum katika hospitali ya kusaidia akina mama kuavya. Wengine wanasema kila Mkenya baada ya hii Katiba kupitishwa, atalazimishwa na Serikali kuwa na ekari moja ya shamba. Hakuna mahali popote katika hii Katiba Kielelezo ambapo pameandikwa kuwa mtu atanyangâanywa shamba lake. Kila Mkenya ambaye ana shamba lake la kibinafsi, ataendelea kumiliki hilo shamba lake. Lakini makabaila, wenye mashamba makubwa makubwa, ya zaidi ya ekari 10,000 peke yao---"
}