GET /api/v0.1/hansard/entries/1053938/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1053938,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1053938/?format=api",
"text_counter": 144,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mvita, ODM",
"speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": "Tatu, kama ni kweli uchunguzi unafanywa mpaka leo, Statement ya Sadat haijachukuliwa. Viongozi wa Wizara hawajui kile ambacho wanachokizungumza. Wamesema kwamba wale ambao walimiminiwa risasi walipelekwa hospitali ya Coast General ambayo ni uongo. Hawakupelekwa huko, Mhe. Naibu wa Spika. Wale waliathirika walipelekwa katika hospitali ya Memon ambayo iko karibu. Baada ya hapo, walipelekwa katika hospitali ya Aga Khan. Wametaja hapa kuwa kuna namba ya Occurrence Book (O.B). Lakusikitisha ni kuwa hakuna mmoja wa wale wanafanya kazi katika eneo hilo, waliopigwa risasi ama familia zao ambao Statement yao zimechukuliwa. Licha ya hivyo, walijipeleka kusema kuwa wanataka kupiga ripoti ya masuala haya. Waliambiwa kuwa ripoti tayari imepigwa, wakae kado."
}