GET /api/v0.1/hansard/entries/1054340/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1054340,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1054340/?format=api",
    "text_counter": 156,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kitutu Chache South, FORD-K",
    "speaker_title": "Hon. Richard Onyonka",
    "speaker": {
        "id": 128,
        "legal_name": "Richard Momoima Onyonka",
        "slug": "richard-onyonka"
    },
    "content": " Asante ndugu Spika. Utaniwia radhi. Ningependa kusema kuwa, kama Mwanachama ambaye yuko katika Kamati ya Bunge ya Bajeti na Uidhinishaji wa Matumizi, tulimuambia Waziri Yatani kuwa sisi tulisikia mawaidha ya Makamu Mwenyekiti, Mhe. Wamunyinyi, aliyemwambia kuwa Wabunge wamesema hawataki kuzungumzia suala la ugavi wa pesa katika nchi hii kama suala la NG-CDF halijazungumziwa. Jambo la pili ni kuwa yale tuliyazungumzia ni kuwa hata mawaidha ya wale Wenyeviti wa Kamati ambao walikuwa wameleta Mswada kujadiliwa na kuzungumzia vile pesa za Serikali zinagawanywa hayakusikizwa. Jambo la tatu ni kuwa Mwenyekiti wetu wa Bajeti na Uidhinishaji wa Matumizi, Kanini Kega, alimuambia Waziri “usipoenda uzungumze na Rais umuambie Wabunge hawatapitisha huu Mswada kama hamtabadilisha yale mambo Wabunge wanataka, hatutapitisha huu Mswada.” Kwa hivyo, ndugu Spika, vile wenzangu wamesema, tutawachilia kujadili hili jambo. Tunataka siku karibu tano, sita au saba tuzungumze kati yetu. Tunataka NG-CDF irudishwe, pesa zetu ziletwe halafu tuanze kuzungumzia mambo ya ugavi wa hela zinazoenda kwa kaunti. Hayo mambo yasipofanyika, huu Mswada hautapita. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}