GET /api/v0.1/hansard/entries/1055004/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1055004,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1055004/?format=api",
"text_counter": 265,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mosop, JP",
"speaker_title": "Hon. Vincent Tuwei",
"speaker": {
"id": 13436,
"legal_name": "Vincent Kipkurui Tuwei",
"slug": "vincent-kipkurui-tuwei"
},
"content": "Nami nakuambia kwamba jamii yetu pia itakuunga mkono kwa sababu wewe ndiwe baadhi ya wale wazee kwao tunasema “muacha mila ni mtumwa” kwa sababu ya mila zetu na taratibu zetu kama jamii. Kwa sababu jamii ambayo unatoka imeona kwamba unafaa, tunakuunga mkono na tunakuomba utumie nafasi hiyo kama balozi wa amani kwa sababu una tajriba ya kuwa wakili. Umekuwa hakimu. Umekuwa mwanasiasa. Sasa wewe ndiwe unasimamia Kiti cha Spika katika jamii. Mmetangamana na viongozi wote walio juu yetu kwa njia moja au nyingine—awe Rais, naibu wake au viongozi wa upinzani. Tunakuomba kwamba katika karne hii uwe kiongozi wa matumaini kwetu na kwa Wakenya. Kwamba, kwa wakati wote, uwe mmoja wa wazee wakati heshima ya wazee mashauri inatakikana. Tunakuunga mkono kama Wabunge. Uendelee mbele kuweka Nyumba hii ya Bunge kuwa nyumba ya heshima. Naomba na kusihi viongozi wenzangu kwamba sisi ni mfano mwema ambao wananchi kule nje wanaiga. Tujipe heshima kwa sababu heshima haitatoka kule nje kama sisi hatujiheshimu. Nikimalizia, nashukuru kwa sababu hili limekuja kwa wakati mzuri—kwamba nchi hii inaenda kutafuta uongozi wa Rais wa tano. Tumia nafasi hiyo ukiangalia kwa macho yako kwa upevu na makini ili kiti ambacho utalenga kiwe kile kitatuunga sote. Mwisho ni kwamba, kama unaweza wanasiasa, ni nani mgumu kuliko mwanasiasa? Wewe ndiwe mwanasiasa mkuu. Cha kufurahisha zaidi na kutamausha ni kwamba unaelewa sheria za nchi hii na wewe ndiwe uliweka kidole chako na bongo lako pale. Tunakuomba usimame imara. Viongozi ambao wako hapa na wale ambao wako nje na wananchi wa Kenya wanategemea wewe na sisi viongozi hapa tutoe maamuzi na muelekeo. Hasa kwa wakati huu ambapo kuna manung’uniko hapa na pale ya Katiba ambayo inatazamiwa kubadilishwa na wengine wanaona kwamba haifai. Tungepewa nafasi sisi kama viongozi tuchangie kwa sababu kwa umoja tutakuwa pamoja na kwa uongozi wako tutakuwa na baraka. Mungu akuzidishie neema na akupe ubora wa afya na upevu mwingi wa fikra na mawazo. Asante sana."
}