GET /api/v0.1/hansard/entries/1055007/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1055007,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1055007/?format=api",
"text_counter": 268,
"type": "speech",
"speaker_name": "Shinyalu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Justus Kizito",
"speaker": {
"id": 71,
"legal_name": "Justus Kizito Mugali",
"slug": "justus-kizito"
},
"content": " Mhe. Spika, japo wengi wamekutolea kongole katika lugha ya Kingereza, ningependa kuongeza sauti yangu nikisema kwamba nakupa pongezi kwa niaba ya watu wangu wa Shinyalu na kongole kwa wewe kutunukiwa nafasi hiyo ambayo ni muhimu katika jamii zetu. Suala la muhimu ni unavyotukalia hapa kama Kinara, unafanya kazi yako sawasawa. Wewe una maingiliano mazuri na Wabunge hawa. Mimi kama Mbunge ambaye amekuwepo hapo awali pia nimeona Spika wengi wakikalia mahali ulipo. Lakini, kwa sasa wewe ndiye mufti na bora zaidi. Ni kwa sababu umeweza kutoa ule ubabe pale. Kuna wale wengine ambao wanakaa pale na ubabe. Wewe umekuwa ni mtu mvumilivu, mzuri, mwenye maingiliano mazuri na Wabunge na pia tunakaa mahali pamoja, tunakula pamoja na tunazungumza pamoja. Hilo ndilo suala ambalo nakuambia kwamba huo ndio uongozi. Suala hilo ndilo limekupa kipaumbele na watu wa kwenu wakaona kwamba watosha. Nami najua kwamba hata sisi katika Mkoa wa Magharibi tunakutambua. Umefanya kazi kwingi katika ule uitifaki wako wa kutarazaki katika masuala ya kisheria. Kule kwetu tumeona umefanya kazi nzuri japo, kama ilivyosemekana kule, labda mambo yapo. Lakini, tunajua kwamba pia wewe si mchache katika maingiliano na watu."
}