GET /api/v0.1/hansard/entries/1055009/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1055009,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1055009/?format=api",
"text_counter": 270,
"type": "speech",
"speaker_name": "Shinyalu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Justus Kizito",
"speaker": {
"id": 71,
"legal_name": "Justus Kizito Mugali",
"slug": "justus-kizito"
},
"content": "Kwa hivyo, tunakusifu na tunakutakia kila la heri kwa sababu watu wa upande ule wa mlima hawakukosea. Wewe umejaa tajriba na vilevile una ukiritimba mkubwa sana katika masuala ya kisheria, masuala ya mambo haya ya Kanuni za Kudumu na kadhalika. Tukirudi katika Bunge, wewe umeleta mabadiliko mengi sana katika Bunge hili. Tumeona Kanuni za Kudumu zimekuja katika Kiswahili. Tunaweza kuzungumza kwenye Bunge katika Kiswahili. Hata tumewapiku wale wenzetu wa Tanzania. Kama unavyojua, Kiswahili cha Kenya ndicho cha ustandadi mkubwa. Wewe umetusaidia sana hapo na tumefurahia kwa sababu tuna ule ustandadi sasa. Tunaweza kuzungumza Kiswahili hapa. Tunaweza kusoma mambo mengi katika Kanuni za Kudumu. Kwa hivyo nasema heko na kongole. Hata nikienda kule kwetu nitaweza kuwauliza wale wengine ambao ni wenzetu waige mfano wako. Nasi tukija jaribu zile za mlimamlima, tutaweza kuja kule tumuambie Baba wa kwetu ambaye tunamjua ndiye kiongozi wetu. Tutamuambia “ukienda kule ujue kwamba kuna kigogo na kigogo huyo anaitwa Bwana Muturi”."
}