GET /api/v0.1/hansard/entries/1055140/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1055140,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1055140/?format=api",
    "text_counter": 401,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nominated, JP",
    "speaker_title": "Hon. David ole Sankok",
    "speaker": {
        "id": 13166,
        "legal_name": "David Ole Sankok",
        "slug": "david-ole-sankok"
    },
    "content": " Asante sana, Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ili nichangie Mswada huu wa Narcotic, Drugs and Psychotropic Substances (Control) (Amendment) Bill (National Assembly Bill No.27 of 2020). Mswada huu umekuja wakati ambao unafaa. Naunga mkono Mswada huu mia kwa mia. Vizazi vyetu viko mashakani kwa sababu ya dawa za kulevya, pombe ikiwa moja zao. Watu ambao wamejaribu kutusaidia ni kama Mheshimiwa “Jicho Pevu” ambaye kwa hilo jicho pevu, aliweza kutuelezea kwa kina wale watu ambao wanauza madawa katika nchi yetu, ijapokuwa vitengo ambavyo vinatakiwa kuwakamata na kuwapeleka kortini vilishindwa na ikabidi nchi za ng’ambo ziwashike wale Akasha brothers. Sisi kama walemavu hatujaangaziwa sana katika Mswada huu. Kwa sababu hiyo, nitaongea na rafiki yangu, Mwenyekiti wa Kamati hii, Bwana Koinange, ili tuweze kuangazia maneno ya walemavu. Nambari yetu inaongezeka kila kuchao kwa sababu watu wengine wanavuta bhangi, wanaharibika kiakili, wanatumia dawa kama heroine na kuwa walemavu. Wengine wanatumia dawa za kulevya wakiwa na mimba halafu baadaye, watoto wanazaliwa wakiwa walemavu wa kiakili. Kwa hivyo, tunaongezeka ilhali kilabu chetu huwa kimejaa. Hatutaki kuongeza watu wengine kwa sababu yale manufaa ambayo tumepewa na Serikali hayatutoshi sisi wenyewe, sembuse wale watakaongezeka kushindania hayo manufaa."
}