GET /api/v0.1/hansard/entries/1055142/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1055142,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1055142/?format=api",
"text_counter": 403,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nominated, JP",
"speaker_title": "Hon. David ole Sankok",
"speaker": {
"id": 13166,
"legal_name": "David Ole Sankok",
"slug": "david-ole-sankok"
},
"content": "Tumeangazia sana kuhusu watu ambao wanauza dawa za kulevya lakini hatujaangazia mambo ya jamii ambayo inachangia sana kwa utumizi wa hizo dawa za kulevya. Hatujaangazia mambo ya shuleni ambapo walimu wengine hawafunzi watoto wetu wakati wako nao ili wajikinge kutokana na dawa za kulevya. Sababu nyingine ni jamii ambayo haina kiongozi. Nasihi akina dada kuwa wakati mwingine, hata kama dada hajaolewa, atafute mjomba ili ahakikishe kuwa watoto wake wamelelewa kwa njia inayofaa. Wakiwa na tabia nzuri ama wamelelewa vizuri, watakuwa wazuri, wangwana na watakataa hata hizo dawa za kulevya wakiletewa. Wakikataa, hiyo biashara ya dawa za kulevya itakufia hapo. Nasihi akina dada. Bibilia inasema kuwa mama aolewe na mzee mmoja. Tamaduni zetu pia zinasema hivyo. Lakini wakati ambapo unachanganya kana kwamba hapa uko na mtoto ambaye amezaliwa na Mkisii, mwingine na Mmasaai, mwingine na Mjaluo, huo mchanganyiko maalumu ndio huleta confusion na shida wakati mwingine. Jambo hilo husababisha watoto kutoroka na kupatwa na watu hao wanaouza dawa za kulevya. Hata kama jamii haina baba, tafuta mjomba ili awaelezee watoto njia ambayo wanatakiwa kuchukua."
}