GET /api/v0.1/hansard/entries/1055147/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1055147,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1055147/?format=api",
"text_counter": 408,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kikuyu, JP",
"speaker_title": "Hon. Kimani Ichung’wah",
"speaker": {
"id": 1835,
"legal_name": "Anthony Kimani Ichung'Wah",
"slug": "anthony-kimani-ichungwah"
},
"content": " Naibu Spika wa Muda, ninajua ulikuwa unashauriana na Kiongozi wa Walio Wengi kwa hivyo labda hukusikia yale ambayo ndugu yangu, Mheshimiwa Nominee 001, amesema. Amesema kuwa mtoto akichanganyika uzazi awe na baba ambaye ni Mjaluo, mwingine sijui amezaliwa na Mkisii, na mwingine na kabila lingine, hayo ndiyo mambo yanayochangia utumizi wa dawa za kulevya. Sijui ni ushahidi gani alio nao wa kuonyesha kuwa ukichanganya uzazi, utatumia dawa za kulevya kutokana na uzazi ama mambo ya ukabila. Hayo ndiyo mambo tunaomba viongozi kuwa tuwache kuchanganya kila kitu na mambo ya ukabila. Hakuna mtoto ambaye huchagua atazaliwa na baba yupi. Hata Nominee 001, kuna ushahidi kuwa kuna vile ambavyo anahusiana na Mheshimiwa wa Bahati, Kimani Ngunjiri, ilhali yeye amezaliwa kule Narok. Sijui kama ni ushahidi kutokana na utumizi wake mwenyewe ama mambo namna gani. Ningeomba afafanue ama atoe matamshi ya kukejeli wale ambao wamezaliwa kutoka kabila tofauti."
}