GET /api/v0.1/hansard/entries/1056214/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1056214,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1056214/?format=api",
    "text_counter": 459,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mohamed Ali (",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Nyali, Independent): Shukrani sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwanza, ningependa kuipongeza Kamati ya Utawala na Usalama wa Taifa kwa kazi nzuri waliofanya. Labda, watu hawajui kwamba mimi ndiye mmiliki wa mapendekezo ya hizi sheria kabla hazijawasilishwa katika Kamati ya Utawala na Usalama wa Taifa. Ninawashukuru kwa sababu wamezingatia yale yote tuliyoyasema. Nami ninaunga mkono kabisa. Tatizo la mihadarati limekuwa donda sugu hususan katika eneo la Pwani. Tulipokuwa tukiangalia sheria za hapo awali na hizi mpya, kulibaini wazi kuwa sheria zilizokuwa zikitumika hapo awali hazikuwa nzito kiwango cha kuwazuia walanguzi kuleta madawa humu nchini. Ningependa kuzizungumzia hizi sheria ambazo zimekuwa kali zaidi. Ni sheria ambazo tumeweza kuzigawanya kwenye njia tatu. Hapo awali, mlanguzi wa madawa ya kulevya na mtumizi walikuwa wakihukumiwa kifungo kimoja, hukumu moja. Sasa, imebainishwa kuwa mtumizi, anayeuza na mlanguzi, kila mmoja wao yuko na hukumu yake. Jambo muhimu katika sheria hii ni kuhakikisha kuwa wale ambao wametumia nguvu za mapeni kuweza kutawala anga na kuhakikisha watoto wetu wanafariki, wanachukuliwa hatua kali ya kisheria. Hii sheria, hakika, inaweza kuwalinda Wakenya na watoto wetu kwa jumla. Polisi sasa wako na sheria itakayomuadhibu atakaenda kinyume na sheria. Walanguzi wa madawa ya kulevya na watumizi wako na sheria yao kila mmoja. Labda, kulikuwa na mtafaruku hapo awali wa kusema The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}