GET /api/v0.1/hansard/entries/1056215/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1056215,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1056215/?format=api",
"text_counter": 460,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mohamed Ali (",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kuwa zile faini zilizowekwa hususan kwa watumizi wa bangi na cocaine, ni kana kwamba wamefinyiliwa sana. Lakini, imepunguzwa kutoka ile pesa ya shilingi milioni ishirini na kifungo cha miaka mitano na kuletwa chini kabisa. Katika siku za usoni, wanasayansi wanasema kuwa inaweza kutumika kama matibabu ya saratani. Ninaunga mkono na ninasema kuwa yeyote atakayepinga swala hili ni adui wa nchi. Hii ni kwa sababu watoto wanaumia, wanakufa kila kukicha na Serikali sasa imepewa nguvu maradufu ya kuweza kunakili kuingia katika nyumba na kupata ushahidi wa sauti na video na kuutumia katika mahakama. Swala la kuwaondoa hapa nchini na kuwapeleka nje ni sawa kabisa. Hii ni kwa sababu lau kama tungeeendelea kukaa katika huu uongozi wetu, yale yaliyopata Bwana Akasha hayangelimpata. Angezidi kuendelea kufanya yale aliyoyafanya humu nchini. Kwa hivyo, hii sheria ya kuweza kubadilishana kimawazo, kama kuna Mkenya anauza madawa ya kulevya hapa nchini Kenya na amepotelea Tanzania ama taifa lingine, Serikali ina haki ya kuzungumza na Serikali ya huko na kuhakikisha kuwa ameletwa humu nchini ili aweze kupata adhabu ya kuangamiza watoto wetu. Ninafurahia vile Kamati hii ilivyofanya kazi yake. Namuona ndugu yangu, Mhe. Kaluma hapa. Wamefanya kazi nzuri, na natumai hii sheria itatumika kuhakikisha kwamba matatizo ya dawa za kulevya, ambayo yamekuwa donda sugu tangu jadi, yamefika mwisho. Ukiangalia matatizo ya dawa za kulevya, zikiwemo cocaine na heroine, yanashuhudiwa Mombasa na katika eneo zima la Pwani kwa jumla. Huwezi kupata mteja Nairobi, Kisumu, Bonde la Ufa ama kwengineko. Wote wanaangamia kupitia sehemu ya ukanda wa Pwani. Hapo, ndipo hizo dawa zinaingilia. Vile vile, sheria hii itahakikisha kwamba yeyote anayesimamia, kwa mfano, Bandari ya Pwani ama sehemu zote ambazo ni za kuingia katika Jamhuri ya Kenya, yeye binafsi, ndiye atakayechukuliwa hatua za kisheria. Hii ni kwa sababu wananchi na Serikali ya nchi imeweza kumpa nafasi hiyo kuhakikisha kwamba hizi dawa haziwezi kuingia tena. Hizi dawa zikiingia, ni sharti, kama ni mkurugenzi wa Halmashauri ya Bandari nchini (KPA), ni lazima aeleze zimepita vipi Pwani na kuingia hadi Nairobi ama sehemu nyingine. Kama ni katika mipaka yetu, kwa mfano Namanga na Malaba, ni lazima pia aeleze ni vipi dawa hizi zimeingia. Vile vile, sheria hizi zimewapa polisi nguvu ya kutosha. Hapo awali polisi walikuwa wakiwashika walanguzi na kuwafikisha mahakamani, lakini ilikuwa zile hadithi za lelemama. Unafika pale, mambo yanapotelea mbali kwa sababu ya nguvu za kazi. Serikali sasa inaweza kushikilia mali ya mlanguzi wa dawa za kulevya hadi pale mahakama itakapomtangaza kuwa ni mtu msafi ndiyo arudishiwe mali yake. Hii itawazuwia walanguzi wa dawa za kulevya kuwekeza pesa katika biashara. Wanawekeza katika mijengo na mataifa ya nje. Hii sheria itaipa Serikali nguvu ya kufuata pesa hizo. Pia, tumependekeza kuwa hizo pesa zikipatikana zitumike kujenga rehabilitation centres ambazo zitakomboa watoto wetu na kuwarudisha katika hali ya kawaida. Nitamalizia kwa kusema kuwa yeyote atakayepinga hii sheria mpya ni adui wa taifa na watoto wetu na anafaa azuiliwe katika kila njia kuhakikisha watoto wetu wanapumua na dawa za kulevya hazimo. Tunataka kuona Kenya ikiwa kama mataifa mengine kama vile Malaysia na Singapore. Ukienda kule na upatikane na gramu hata moja ya dawa za kulevya, hukumu ni kifo. Serikali za zile nchi zinawekeza katika watoto wao na kuwalinda pia. Tunataka kuwa na hizi sheria kali ili tuweze kuwekeza katika afya bora na watoto ambao wako na akili na fikira za kuikomboa nchi hii katika siku za usoni. Tusiwekeze kwenye watoto ambao wamegeuzwa na kuwa mazezeta wasiojua mbele wala nyuma. Maisha yao yatakuwa vipi kwa sababu ya dawa ya kulevya? Pindi tu hii sheria The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}