GET /api/v0.1/hansard/entries/1056216/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1056216,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1056216/?format=api",
"text_counter": 461,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mohamed Ali (",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "itakapopita, pia tunataka kuona asasi zote za usalama nchini Kenya zikichukua hatua. Hapo awali, walikuwa wakisema hii sheria sio kali, hailindi na inafaa kubadilishwa. Sasa hivi, Bunge hili, kwa heshima ya Kamati ya Utawala na Usalama wa Taifa, limeweza kuleta hii sheria ili iweze kupitishwa. Sasa tunataka kuona maafisa wa kulinda usalama katika asasi zote wameanza kufanya kazi. Hatutaki hao samaki wadogo watumizi, tunataka walanguzi wa dawa za kulevya. Hapa Kenya hawako wengi. Wakati mmoja miaka ya nyuma, mambo mengi yalizungumzwa katika Bunge hili. Ni sharti Serikali ya hii nchi, kupitia asasi za usalama, kusimama kidete na kutumia sheria hizi mpya ambazo zimeletwa kukinga watoto wetu na kuhakikisha kwamba kwenye ukanda wa Pwani na Kenya nzima, suala la madawa ya kulevya halimo tena. Ukiangalia maswala hayo ya madawa ya kulevya, yamevuka mpaka sasa. Watoto wanakimbilia dawa zingine za kujichanganyishia kama vile codeine. Watoto pia wanakula muguka na wanatumia kila aina ya dawa za kulevya. Ni lazima katika hii nchi tuwe na utaratibu wa kuwakinga watoto wetu. Ni lazima kuwepo na sheria ambazo zitalinda maslahi ya watoto wetu kwa sababu nchi ambayo inazalisha ujinga itatawaliwa na ujinga miaka nenda miaka rudi. Lakini nchi ambayo imeekeza katika elimu ya watoto wake, na inayowekeza na misingi bora, inakuwa kiafya, kimiundo misingi na nguvu kazi. Kule Mombasa ama katika sehemu za ukanda wa Pwani, vijana wote hawana kazi. Asilimia kubwa ya vijana wanatumia madawa ya kulevya. Ni kwa sababu tumeshindwa kuwapa nafasi ya kuelekeza fikira zao kwenye elimu, katika miundo misingi na kwa nguvu kazi. Hii sheria ambayo imeletwa ni nzuri sana. Itahakikisha hayo yote tunayozungumzia yataisha. Nataka kumwona Mhe. mwenzangu, Kaluma, atakapotembea katika sehemu za ukanda wa Pwani, awe anaona kuwa mambo ni shwari na sisi sote tutafurahi pamoja na kulinda heshima ya watoto wetu. Kwa hayo machache, ninaunga mkono. Asante sana kwa huu uhusika wote. Shukrani Naibu Spika wa Muda."
}