GET /api/v0.1/hansard/entries/1056262/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1056262,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1056262/?format=api",
"text_counter": 507,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Janet Nangabo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": "Vile wanenaji wa kwanza wamesema, ni kweli watoto wetu na watu wa rika zetu wameumia. Iwapo sheria kama hii italetwa katika Bunge letu ama nchi yetu, tutazuia hao wakora ama wahalifu ambao wanakuja kunyanyasa watoto wetu. Hao watu wanalenga vyuo vikuu katika nchi yetu ya Kenya. Hivi majuzi, mama alitafuta mtoto wake kwa miaka miwili na kumbe alikuwa ameharibikia hapa katika kaunti ya Nairobi. Watoto wetu wamekuwa wateja wao wa kuwaletea hii mihadarati. Nimefurahi kwa sababu Kamati imeweka faini ya kuhakikisha kwamba walanguzi na wanaotumia dawa za kulevya hawataenda nje ya mkono wa sheria. Watashikwa, kushtakiwa na kutoa faini ya Ksh 20 milioni."
}