GET /api/v0.1/hansard/entries/1056266/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1056266,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1056266/?format=api",
    "text_counter": 511,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Janet Nangabo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1076,
        "legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
        "slug": "janet-nangabo-wanyama"
    },
    "content": "Waheshimiwa wameongea kuhusu maofisa ambao wanafaa washike doria ama kuchunguza hao watu wa kuleta mihadarati. Wenzangu wamesema kwamba hapo awali kulikuwa na wale wanatengeza biashara. Wakipata hii mihadarati na kuuza, wanapewa kitu kidogo. Kwa sababu tunaweka hii sheria saa hii, hata hao askari wataogopa. Wakipatikana, watapoteza kazi na hata wengine pia watafungwa jela. Hii sheria italeta manufaa katika nchi yetu ya Kenya. Itafanya sisi, kama viongozi katika Bunge hili, tuhamasishe watu kule nje. Wengine hawatajua kwamba tuko na sheria kama hii na mwishowe watatumia watoto wetu. Nilishukuru sana Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama, Mhe. Koinange leo asubuhi. Alisema kwamba wanaoendesha boda boda watakuwa na mafunzo. Wataangalia vile wanaendesha hizi boda boda, kwa sababu hao walagunzi wa dawa za kulevya hawatumii magari saa hizi. Wanachukua watu ambao wanaendesha boda boda . Huyu anabeba anafikisha mahali fulani na mwingine anapeana kwa mwingine."
}