GET /api/v0.1/hansard/entries/1057879/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1057879,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1057879/?format=api",
    "text_counter": 82,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Mwaura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13129,
        "legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
        "slug": "isaac-mwaura"
    },
    "content": "Asante sana Bw. Spika. Ninaunga mkono Kauli hiyo. Kwa kweli barabara zetu za Kenya, mara nyingi kuna wale wanaoshinda hizo zabuni lakini wanachukua muda mrefu sana kuzijenga na hususan makadirio ya fedha ambazo zinatengwa zinapita kipimo. Kwa mfano utakuta barabara zingine zinajengwa kwa Ksh40 millioni kwa kilomita na zingine zinafika mpaka billioni moja. Maendeleo ni sawa lakini ni muhimu sana isiwe pia ni maendeleo ya ufisadi ambayo nia yake ni kuwaibia Wakenya hususan pia tukiangalia muda ambao unachukuliwa kutengeneza hizo barabara. Ni jambo la msingi ambalo linafaa kuangaziwa zaidi. Ninafikiri tunafaa kuwa na ratiba nzuri ambayo inaorodhesha viwango vya fedha zinazofaa kutumika katika ujenzi wa barabaara na muda unaofaa ili wanakandarasi wasikae pale ndani wakifuja pesa za umma ilhali Wakenya wanaendelea kuadhirika. Naunga mkono."
}