GET /api/v0.1/hansard/entries/1059250/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1059250,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1059250/?format=api",
    "text_counter": 84,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii niweze kupongeza Sen. Kavindu Muthama kwa kuchaguliwa kama Seneta wa Kaunti ya Machakos. Watu wa Kaunti ya Machakos wameamua na pia wamesema kwa sauti moja kwamba mama anaweza. Tulikuwa tunatarajia na tumeona mama ametosha kweli. Karibu Sana, Sen. Agnes Kavindu Muthama. Natoa shukrani zangu kwa niaba ya watu wa Kaunti ya Kwale. Shukurani pia zimfikie mkuu wa chama cha Wiper Democratic Movement – Kenya (WDM-K), mhe. Steven Kalonzo Musyoka. Alifanya kazi nzuri sana na kuhakikisha kwamba kampeni imeenda salama na kwa amani. Bw. Spika, ningependa pia kuwashukuru viongozi wengine kama wa Chama cha Jubilee, WDM-K, Amani National Congress (ANC) na Kenya African National Union (KANU) kwa kuungana pamoja katika kampeni. Walifanya kampeni kwa njia ya amani na kuhakikisha kwamba Sen. Agnes Kavindu Muthama ndiye mshindi wa kiti cha Seneta wa Kaunti ya Machakos. Ushindi wake ulikuwa ni mkubwa sana na wa kihistoria. Itakumbukwa kwamba Sen. Kavindu Muthama alipata karibu kura laki moja na zaidi na wa pili wake alipata karibu elfu kumi na saba au elfu kumi na sita. Hii ni kuonyesha kwamba mama anaweza na sisi kama Maseneta, tunasimama naye Sen. Kavindu Muthama. Tutamuunga mkono katika kila jambo katika Seneti hii. Asante sana, Bw. Spika."
}