GET /api/v0.1/hansard/entries/1059542/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1059542,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1059542/?format=api",
    "text_counter": 376,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Mambo ya kisheria lazima yachukue mkondo wake na taratibu za kisheria kufuatwa. Katika mchakato huu, jambo kubwa sana ni kwamba hili ni jambo litakalokuwa sharia ambazo zitatumika katika siku za usoni kusaidia Wakenya. Ningependa kumpa kongole dada yetu, Sen. Agnes Kavindu Muthama, aliyekuja hapa. Yeye ni mama mkakamavu sana. Amedhihirisha wazi kwamba anaweza kuingia katika ulingo wa siasa, kumenyana na wanaume na kuwabwaga. Kongole sana dada yangu kwa kuja hapa Bunge la Seneti. Hili ni Bunge lenye uzoefu mkubwa katika taratibu zake za Bunge. Majadiliano hapa huwa makali na tunakosana lakini mwisho, tunaweka akili pamoja na kuendelea mbele sawasawa. Karibu sana. Bw. Spika wa Muda, tunajua vile sheria zinatakiwa kutengenezwa. Kuna watu ambao hawakuhusishwa ama Wakenya wote wamehusishwa na jambo hili liko Bungeni sasa hivi. Bunge ndio kielelezo kikubwa. Tunajua kuna kule kujumuisha watu wote na kuzungumzia Mjadala kama huu. Sasa imefika wakati ambapo Ripoti imeandikwa na hili Bunge liko na haki kabisa kuweka mchango wake hapo. Muda ambao umeombwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maswala ya Sheria na Haki za Binadamu upewe kipa umbele. Ni muhimu Kamati hiyo ipewe muda kuchambua na ilete ripoti itakayokuwa sawa kisheria na pia itakayokubalika. Baada ya hapo, mambo yote yatakayopelekwa katika kura ya maoni yatakuwa ya kukubalika na Wakenya wote. Ninafikiria ni vizuri muda huo upatikane."
}