GET /api/v0.1/hansard/entries/1059608/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1059608,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1059608/?format=api",
"text_counter": 54,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Hoja hii ya kubadilisha ratiba ya vikao vya Seneti. Ni kweli ugonjwa wa korona umerudi kwa raundi ya tatu kwa vishindo. Raundi hii ni hatari zaidi kuliko raundi zile mbili zilizo tangulia. Wakati ugonjwa huu ulipozuka, Bunge la Seneti lilichagua Kamati ya COVID-19. Kamati ilifanya kazi nzuri sana. Ilikuwa inatoa mwelekeo kila wiki kuhusu kazi yao na vikao vyake na taasi nyingine za Serikali. Bw. Spika, kutoka muhula wa Kamati hiyo kuisha, hakujakuwa na mwongozo wowote katika Bunge hili kuhusiana na masuala ya COVID-19. Ni aibu kwamba mpaka sasa kutoka raundi ya tatu ianze hatujakuwa na mwongozo wowote uliotolewa katika Bunge hii kuhusiana na vipi wananchi watafanya kuepukana na janga hili. Pia serikali za kaunti ziko usingizini. Hakuna mwongozo wowote wa vipi tutajiepusha na maradhi haya kwa raundi nyingine wala kampeni za watu kupokea chanjo. Ni jambo ambalo linaathiri wananchi na wanapoteza Maisha bila kuwa na tahadhari yoyote. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}