GET /api/v0.1/hansard/entries/1059801/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1059801,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1059801/?format=api",
    "text_counter": 247,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Mwaura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13129,
        "legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
        "slug": "isaac-mwaura"
    },
    "content": "Asante Sana, Bi. Naibu Spika. Ningependa kuunga MaSeneta wenzangu kwa kutoa rambirambi zangu na heko kwa Mheshimiwa John Pombe Magufuli ambaye niliwai kukutana naye mara mbili hapa Kenya katika pilka pilka zetu za kisiasa na katika Chama cha Orange Democratic Movement (ODM) wakati nilikuwa mwanachama. Ni Rais ambaye aliwai kutungiwa jina nzuri sana la Magufulify; la kumaanisha kwamba ni ule utendakazi, hapa kazi tu. Ni Rais ambaye alishindana kabisa na rafiki yangu mwingine anaitwa January Makamba na akaweza kuwapiku hata Edward Lewasa kuwa kiongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM). Lakini pia hakuwa Rais peke yake, alikua Mwafrika ambaye alihakikisha kuwa amepigana na ufisadi na rushwa. Fauka ya hayo, alihakikisha kuwa reli ya Standard Gauge Railway (SGR) ya kule haikutumia fedha nyingi sana kama hii ya Kenya. Pia, alihakikisha kuwa barabara zimejengwa kwa bei nafuu. Alikuwa anawaeleza wanakandarasi warudie barabara ambazo ni mbovu. Mimi nimeshabikia hilo katika Jamuhuri ya Tanzania. Kwa hivyo, ni mtu ambaye tunamsifu. Alihakikisha kuwa zile kodi ambazo zilikuwa zinachukuliwa na Taasisi ya Kodi ya Tanzania, Tanzania Revenue Authority, zimeweza kuongezeka mara tatu tangu alipochukua usukani."
}