GET /api/v0.1/hansard/entries/1059805/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1059805,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1059805/?format=api",
"text_counter": 251,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Mwaura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13129,
"legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
"slug": "isaac-mwaura"
},
"content": "kwamba tunapatia wenzetu malighafi na mwishowe tunapata bidhaa ambazo zimetengenezwa na ni mali yetu. Bi. Spika wa Muda, ningependa kusema kwamba ni vizuri kumsifu Suluhu Salma kwa sababu yeye ni mwanamke wa kwanza kuwa Rais Tanzania. Kuna mambo yake mengi ambayo yanatajika. Rais Magufuli hakuwa na haki mzuri katika haki za kibinadamu. Rafiki yangu, mhe. Tundu Lissu, yuko Ubelgiji kwa sababu ya kupigwa risasi kumi na sita (16). Mungu amsaidie. Wiki hii, anatibiwa mkono wake kutokana na tukio hilo. Tanzania, chini ya Rais Magufuli, haikuwa inawajibika katika haki za kibinadamu. Watu waligandamizwa, wengine wakapotea na upinzani ukanyanyaswa sana katika uchaguzi uliopita hivi kwamba Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiliweza kupata Wabunge wawili pekee. Wale ambao ni wa kuteuliwa ambao ni kina mama, viti mia moja kumi na tatu (103), wakapatiwa kwa nguvu viti kumi na tisa (19). Nafikiri kuwa hili ni swala kubwa. Niliskia Sen. Orengo akisema Xi Jinping lakini DengXiaoping. Unawezaje kutawala nchi bila ubepari? Unawezaje kuhakikishwa kuwa unafanya maendeleo pasipo na kugandamiza haki za kibinadamu? Je, ni rahisi kuwa na dhana mbadala ambazo zitakuwezesha kuwa na maoni tofauti ya utenda kazi na sera ya kiserekali? Nafikiri hilo ni jambo ambalo wale ambao ni wanafalsafa ambao ni wasomi wa siasa wataweza kuangazia wakati ambapo tunatathmini maisha ya mwendazake Marehemu Hayati John Pombe Magufuli. Kwa ujumla, tunamsifia Hayati (Dkt.) John Pombe Magufuli kwa sababu alikuwa amejitolea kama kiongozi wa Afrika. Hata, alikuwa amewashawishi Watanzania kutumia tiba za kiasili kutoka kule Madagascar, hata isipokuwa rafiki yangu, Augustine Mahiga, aliye kuwa Waziri Mkuu, alikufa kutokana na ugonjwa wa COVID-19. Hayati (Dkt.) John Pombe Magufuli ni mtu ambaye alikuwa mtanashati. Alikuwa na umahiri na ushupavu wa kuhakikisha kwamba Uafrika umeithinika. Alikuwa amekataa kupata hii chanjo rasmi dhidi ya COVID-19 kwa sababu alikuwa anasema pengine kuna mambo yasiyoeleweka mle. Kwa ujumla, hayati Rais, alikuwa ni mtu ambaye amejitolea. Tunamsifu, sio kwa sababu ya kuwa na tathimini moja tu yake. Tuangalie mazuri yake na pia yale ambayo pengine hakufanya vizuri. Hii ni kwa sababu pia yeye ni binadamu na tunajua kwamba hakuna binadamu ambaye hana dosari. Kwa hayo mengi na machache, Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi na tutumie muda huu kusema kwamba dini itumiwe kwa haki na sio kukandamiza watu. Isitumiwe tu kwa kigezo ili uweze kushinda uchaguzi. Ni vizuri kutumia dini kuhakikisha kwamba watu wote wanajumuishwa kwa pamoja. Kwa hivyo, nauungana na wenzangu kutoa rambirambi hizo."
}