GET /api/v0.1/hansard/entries/1059821/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1059821,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1059821/?format=api",
    "text_counter": 267,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda. Kwa niaba wa watu wa Kilfi, na kwa niamba yangu, ningependa kutoa rambirambi zangu za dhati kwa watu wa Tanzania. Watu wa Tanzania wamekumbwa na jonzi juu katika maisha yao. Kama tunavyojua, Rais John Pombe Magufuli alijulikana kwa vitendo. Kwa sababu hiyo, ni Rais aliyependwa na wengi. Alipendwa na watu kwa sababu ni mtu aliyekuwa anasimama na wanyonge na maskini kabisa wa Tanzania. Nakumbuka nikimwona akienda kwa fundraising ya kanisa. Yeye mwenyewe ndiye alikuwa anatembea na bakuli akiwaambia watu wachange ili kanisa lipate kujengwa. Ni jambo la kupendeza sana, na ni mfano wa kuiga. Alikuwa Rais wa vitendo kwa sababu hivi leo, ukienda Tanzania, utaona kwamba Watanzania wameendelea sana. Alipokuwa Rais, alianzisha Tanzanian Airways, kitu kilichokuwa kimekufa zamani. Aliianzisha na aliwaeleza Watanzania kwamba wanaweza kujivunia na ndege zao za Tanzanian Airways. Hilo likikuwa jambo kubwa na la kupendeza kwa Watanzania. Vile vile, alitengeneza barabara katika Jiji la Dar-es-Salaam zinazoitwa mwendo kasi. Mimi sijaona mfano kama huo. Hizo ni basi ambazo ziko na barabara zao katikati mwa mji. Ni basi peke yake ndizo zinapita hapo, na zinapita kwa hali ya kasi sana. Hakuna kuchelewa ukienda kazini. Hilo pia ni jambo aliloweza kufanikisha ndani ya Tanzania. Bi. Spika wa Muda, aliweza pia kupanua airport ya Dar-es-Salaam, na pia akaanzisha airport nyinyine. Tanzania imekuwa na maendeleo. Wako na ndege zao na viwanja vya ndege. Hayo ni maendeleo. Kuna mambo mengi yanaweza kusemwa kuhusu Rais Magufuli. Yeye alikuwa mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM). Yeye mwenyewe aliishi kufanya mapinduzi ya maendeleo kwa kuchukua mstari wa mbele kuona kwamba Watanzania walikuja kwanza katika maisha yake kuliko yeye binafsi. Hilo ni jambo la kijivunia kama Rais."
}