GET /api/v0.1/hansard/entries/1059847/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1059847,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1059847/?format=api",
    "text_counter": 293,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Cherargei",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13217,
        "legal_name": "Cherarkey K Samson",
        "slug": "cherarkey-k-samson"
    },
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda. Kwa niaba yangu, familia yangu na wakaazi wa Kaunti ya Nandi, ningependa kuchukua fursa hii kutoa risala za rambirambi kwa jamii, familia na wananchi wote wa Tanzania, kwa kumpoteza Rais wao mchapa kazi, Rais John Joseph Pombe Magufuli. Msiba huo ulitupata kwa mshtuko sana, ikizingatiwa Rais Magufuli alichaguliwa kwa kipindi cha pili na cha mwisho kama Rais wa awamu ya tano ya Taifa la Tanzania. Nina mambo mawili tu ambayo ningependa kutaja kumuenzi na kumsifu Rais Hayati Magufuli. Kwanza ni kuhusiana na maswala ya madini. Nilifurahi nilipoona akipambana na wale waliyokuwa wakitoa madini katika taifa la Tanzania bila kutoa ushuru kwa maendeleo ya wananchi wa Tanzania. Hatua hii ilinifurahisha sana kwa sababu katika taifa letu la Kenya, kuna kampuni nyingi za kigeni ambazo zinatoa madini bila kutoa ushuru kusaidia maendeleo na pia kuhakikisha utunzi wa mazingira. Pili, Bi Spika wa Muda, ni kuomba mikopo kutoka mataifa ya ng’ambo. Ninamshukuru Hayati Rais Magufuli kwa kuhakikisha zile pesa zilizokusanywa katika Taifa la Tanzania The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}