GET /api/v0.1/hansard/entries/1059848/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1059848,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1059848/?format=api",
"text_counter": 294,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Cherargei",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13217,
"legal_name": "Cherarkey K Samson",
"slug": "cherarkey-k-samson"
},
"content": "ndizo zilizotumika katika ujenzi wa miundomsingi. Tumeona reli ya kisasa na maendeleo mengine. Wengi wamesema uongozi wake haukukubalika sana. Ninafikiri tu ni ukandamizaji wa haki za kibinadamu na pia kujaribu kuzuia demokrasia. Ninafikiri Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan atajaribu kurekebisha na kuleta umoja, uwiano na maendeleo nchini Tanzania. Jambo ambalo linilishtua ni kwamba Hayati Rais Magufuli alikuwa mwanasayansi lakini hakushughulikia janga la Corona kulingana na maelekezo ya kisayansi. Ninamuomba Mhe. Suluhu, Rais mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ashughulikie swala hilo kwa uzito sana. Mazishi yatakapomalizika kesho au kesho kutwa kwa mbashara, tunawatakia familia yake na wananchi wa Tanzania kila la kheri. Mwisho, Bi Spika wa Muda, ningependa kuchukua nafasi hii kumpongeza Sen. Madzayo ambaye amechaguliwa kuwa Naibu wa Kiongozi wa walio Wachache katika Bunge la Seneti. Yeye ni rafiki yangu sana na ninamtakia kila la kheri. Ni mtu mtulivu sana aliyefanya kazi kwa muda mrefu na ana hekima. Unapoona alivyotulia, ni kiongozi ambaye ninatarajia atatusaidia kuongoza Bunge la Seneti, hasa tunapomaliza awamu ya mwisho kabla ya uchaguzi wa mwaka wa 2022. Tunakutakia kila la kheri. Na kama wale Walio Wengi Bungeni, tunatarajia uongozi wako utakuwa wa kuleta umoja na uwiano ili twende mbele. Nina matumaini kwamba Naibu Kiongozi wa Walio Wachache atafanya kazi na wewe ili kuleta uongozi bora katika Bunge la Seneti."
}