GET /api/v0.1/hansard/entries/1059850/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1059850,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1059850/?format=api",
    "text_counter": 296,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda. Ninasimama nikiwa na masikitiko na mshangao kwa kumpoteza kiongozi ambaye tulimuenzi sana sisi Waafrika, Hayati John Pombe Magufuli. Ni mtu ambaye tulimjua na tulijua kauli yake mbiu huko Tanzania ni kusema “Hapa kazi tu”. Ninakumbuka vizuri hata Gavana wa Kaunti ya Murang’a alimuiga na kutumia lugha ya Kikuyu na kusema “Nowera tu”. Tunajua alifanya kazi kwa kujitolea. Alipigana kimasomaso na ufisadi na kusema hatakubali mtu yeyote avune mahali ambapo hakupanda. Kwa hivyo, tunamuenzi na tutamkosa sana kwa sababu alijitolea kiwango ambacho viongozi wengi hawajafikia. Bi Spika wa Muda, kwa miaka mitano aliyoongoza, uchumi ulibadilika. Alikuwa ametegemea kwamba mwaka wa 2025 atakuwa amefika kiwango fulani. Alikifikia kabla wakati huo haujafika. Alikuwa kiongozi ambaye kila mtu hapa Afrika angependa kumuenzi. Yeye hakupendelea sana mambo ya mikopo na mambo ya kusafiri. Kwa hivyo, ni vizuri ijulikane wazi kwamba Mwafrika anaweza. Tunajua ya kwamba Rais Suluhu atajitolea na atafanya mengi. Bi. Spika wa Muda, ninampongeza mwenzangu, Sen. Madzayo, ambaye amechaguliwa kuwa Naibu Kiongozi wa Walio Wachache. Ninajua amebobea katika kazi yake. Ninajua atafanya kazi bila mapendeleo yoyote. Hii ni kwa sababu ninamjua kama mtu anayefanya jambo kwa weledi na ustadi. Ninajua ya kwamba atafanya Bunge hili liwe kitu kimoja kwa sababu anajua, umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}